Mwanadada ajifungua watoto watatu, aomba msaada baada ya mpenziwe kutoroka

Muhtasari

•Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21 alijifungua watoto hao watatu kwa njia ya upasuaji (CS)

•Minoo aliwaambia waandishi wa habari kwamba baba wa watoto wake alitoweka punde alipogundua kuwa ni mjamzito.

Mercelina Minoo akiwa na watoto wake watatu katika hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Ijumaa, Machi 25, 2022.
Mercelina Minoo akiwa na watoto wake watatu katika hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Ijumaa, Machi 25, 2022.
Image: GEORGE OWITI

Familia moja kutoka eneo la Tala, Kaunti ya Machakos inasherehekea baada ya binti yao Mercelina Minoo kujifungua watoto watatu.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye sasa ni mama asiye na mume, alijifungua watoto hao watatu kwa njia ya upasuaji (CS) katika Hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Machi 10.

Minoo ametoa ombi la msaada wa kifedha ili kuweza kuwalea watoto wake wachanga.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba baba wa watoto wake alitoweka punde alipogundua kuwa ni mjamzito.

"Ninatoka katika familia masikini kwa hivyo naomba usaidizi kutoka kwa wasamaria wema ili kulea watoto wangu. Wazazi wangu ni wakulima wadogo ambao hawana uwezo wa kunisaidia kulea watoto kwa vile wana majukumu mengine,” Minoo alisema.

Mercelina Minoo akiwa na watoto wake watatu katika hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Ijumaa, Machi 25, 2022.
Mercelina Minoo akiwa na watoto wake watatu katika hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Ijumaa, Machi 25, 2022.
Image: GEORGE OWITI

Wazazi wa Minoo walisema watamkaribisha binti yao nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini

Muuguzi Esther Nzioki, ambaye alimhudumia Minoo hospitalini alisema anaendelea vizuri baada ya kujifungua.

"Watoto wamekuwa wakiendelea vyema tangu walipoletwa kwenye chumba cha watoto," Nzioki alisema.

Mtoto wa kwanza alikuwa na uzito wa gramu 18.9, wa pili Kilo 2, na wa tatu alikuwa na gramu 15.

Watoto watatu wa Mercelina Minoo katika hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Ijumaa, Machi 25, 2022
Watoto watatu wa Mercelina Minoo katika hospitali ya Kangundo Level 4 katika Kaunti ya Machakos mnamo Ijumaa, Machi 25, 2022
Image: GEORGE OWITI

Nzioki alisema mtoto huyo wa tatu alikuwa ameongeza uzito kutoka gramu 15 hadi 16.40.

"Siku zote tunawaruhusu watoto wenye uzito pungufukuondoka hospitalini baada ya kufikia gramu 18. Minoo ana mama anayemsaidia. Ni sharti akule nyama nyingi ambazo mama yake  amekuwa akimletea hospitalini. Hii ndiyo sababu anaendelea vyema na watoto wanapata maziwa ya kutosha kutoka kwake,” alisema.