Wazazi wapya mjini! Nadia Mukami na Arrow Bwoy wabarikiwa na mtoto wa kiume

Muhtasari

•Arrow Bwoy alitaja mwanao kama zawadi nzuri kuwahi pokea maishani.

Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAMI

Wanandoa mashuhuri Nadia Mukami na Arrow Bwoy wamemkaribisha mtoto wao wa kwanza duniani.

Nadia alijifungua mtoto wa kiume mnamo siku ya Alhamisi, Machi 24.

Wakithibitisha habari hizo njema kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wawili hao wao walifichua kuwa jina la mwanao Haseeb Kai.

"Karibu katika ulimwengu wetu Haseeb Kai. Machi 24, 2022," Nadia aliandika chini ya picha iliyoonyesha akiwa amelala katika wodi ya uzazi na mumewe kando yake akiwa amemshika mtoto wao mikononi.

Image: FACEBOOK// NADIA MUKAMI

Arrow Bwoy alitaja mwanao kama zawadi nzuri kuwahi pokea maishani.

"24.03.2022 tumepokea zawadi nzuri zaidi Haseeb Kai. Karibu kwenye ulimwengu wetu," Arrow Bwoy aliandika.

Wazazi hao wapya tayari wamefungulia mtoto wao ukurasa wa Instagram ambao umeweza  kujizolea wafuasi zaidi ya elfu nne.