Jamaa aua mkewe kwa kumkata koo na kuacha ujumbe "Alinisaliti"

Muhtasari

•Maafisa wa polisi wanaamini kuwa huenda mshukiwa alimuua mpenzi wake kufuatia mzozo wa kimapenzi.

•Polisi walipata barua inayoaminika kuandikwa na mshukiwa na kuachwa kwenye mwili wa marehemu kabla ya kutoweka.

Crime scene
Crime scene

Wapelelezi wa DCI katika Kaunti ya Machakos wanachunguza kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 22 anaaminika kuua mpenziwe katika kaunti ndogo ya Kathiani.

Mshukiwa anaripotiwa kumuua mpenzi wake wa miaka 21 kwa kumkatakata kutumia kisu cha jikoni kabla ya kwenda mafichoni. Polisi walipata silaha mauaji kwenye eneo la tukio.

Polisi wanaamini kuwa huenda mshukiwa alimuua mpenzi wake kufuatia mzozo wa kimapenzi.

"Mwanamume huyo alimkata koromeo mpenzi wake na kumchoma kisu hadi kufa. Mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha makubwa kifuani na usoni," Polisi mmoja alisema.

Mwili wa mwanamke huyo uligunduliwa na majirani ambao waliripoti kisa hicho kwa polisi.

"Tuliamshwa na harufu mbaya iliyokuwa ikitoka kwa nyumba ya mshukiwa," Jirani mmoja aliwaambia wanahabari.

Polisi walipata barua inayoaminika kuandikwa na mshukiwa na kuachwa kwenye mwili wa marehemu kabla ya kutoweka.

"Alisababisha kila kitu na Alex kutoka Kiteini, alinisaliti. Sikuweza kustahimili, alivunja agano letu. Tulikuwa tumekubaliana kwamba mtu yeyote asimsaliti mwingine na ikitokea basi afe au wote wawili wafe," Sehemu ya barua hiyo ilisoma..

"Kila mtu atanilaani lakini niko sawa kabisa, kwaheri. Pole kwa kila mtu, mlaumu Alex, alijua kila kitu kutuhusu,"Barua ilisoma.

Mwili huo ulitolewa na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Machakos Level 5 ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Maafisa wa DCI wameanzisha msako dhidi ya mshukiwa huyo