"Anapenda wanawake sana!" Eudoxie afichua chanzo cha misukasuko katika mahusiano na Grand P

Grand P alifichua kuwa nia yake ni kuoa takriban wanawake wanne.

Muhtasari

•Eudoxie Yao alifichua kuwa amewahi kuachana na Grand P na kurudiana naye mara kadhaa tangu waanze kuchumbiana.

•“Nataka kuoa wanawake wanne. Si mimi niliyesema hivyo, ni baba yangu (Mungu) anayesema hivyo,” Grand P alisema.

Grand P na Eudoxie Yao
Grand P na Eudoxie Yao
Image: INSTAGRAM

Mwanasholaiti maarufu wa Ivory Coast Eudoxie Yao ambaye anajulikana sana kwa umbo wake uliopinda amefunguka kuhusu sababu ya misukasuko mingi katika uhusiano wake na mwimbaji wa Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P .

Katika mahojiano na kituo cha runinga cha Ghana, Joy News, mrembo huyo alifichua kuwa amewahi kuachana na Grand P na kurudiana naye mara kadhaa tangu waanze kuchumbiana takriban miaka minne iliyopita.

Alidai kuwa mwanamuziki huyo bwenyenye ana upendo mkubwa kwa wanawake, jambo ambalo limemfanya amuache mara kadhaa wakati wa uhusiano wao.

"Tumechumbiana tangu 2019. Tunaachana, Tunarudiana. Tunaachana tena na kurudiana.. Anapenda wanawake sana,” Grand P alisema.

Grand P ambaye alikuwa pamoja na mpenzi wake wakati wa mahojiano hayo hata hivyo alikuwa mwepesi sana kukanusha madai ya kuwapenda wanawake sana.

"Hapana! Hapana! Ni Mungu pekee ndiye anayejua,” Grand P alisema.

Huku akizungumzia uhusiano wao, Bi Yao aliweka wazi kuwa licha ya wao kutofunga ndoa rasmi, upendo  ni wa kweli kabisa.

Wakati wa mahojiano, Grand P ambaye ni Muislamu hata hivyo alifichua kuwa nia yake ni kuoa takriban wanawake wanne.

“Nataka kuoa wanawake wanne. Si mimi niliyesema hivyo, ni baba yangu (Mungu) anayesema hivyo,” alisema.

Eudoxie Yao hata hivyo alikuwa mwepesi wa kutokubaliana na wazo hilo akisema, "Ikiwa atathubutu, tunaachana."

Grand P hata hivyo alidokeza kuwa hataogopa sana kumpoteza mwanamke huyo mwenye umbo wa kupinda ambaye amechumbiana naye kwa miaka minne iwapo ataamua kuachana naye.