'Kabla hujamuoa mrembo hakikisha anakufumani na mrembo mwingine angalau mara mbili'

“Kwa njia hiyo utakuwa na uhakika zaidi kama mwanamke unayetaka kumuoa ana hofu ya Mungu na moyo wa kusamehe. Mapenzi ya dhati ni lazima kusameheana,” aliongeza.

Muhtasari

• Alisema kwamba hicho kinafaa kuwa kipimo si tu cha mapenzi bali pia kuangalia kama amekomaa katika kuwa na hofu ya Mungu na pia kuwa na moyo wa kuweza kusamehe.

Adai kabla ya kumuoa mrembo wake kwanza akufumanie
Usman Ahmad// Adai kabla ya kumuoa mrembo wake kwanza akufumanie
Image: Facebook

Kijana mmoja kwa jina Usman Ahmad amezua mjadala pevu katika mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba mwanamume kabla hajamuoa mrembo yeyote yule anayekusudiwa kumfanya mke wake, sharti ampime Imani yake ya uvumilivu iko katika kiwango kipi.

Kwa mujibu wa Ahmad, kipimo chenyewe ni kujiweka katika mazingira ya mrembo huyo kukufumania wewe kama mwanamume, angalau mara mbili ili kuona jinsi atakavyochukua na kulitafutia ufumbuzi suala zima.

Ahmad alisema kwamba hapo ndipo utapata picha halisi ya mwanamke unayekusudia kuishi naye katika ndoa kama ni mtu muelewa ama ni yule wa kukurupukia mambo kwa kuendekeza hisia na hasira badala ya kutumia busara kulitatua.

Mwanaume kabla hujaoa mwanamke yeyote yule hakikisha unayetaka kumuoa anakufumania angalau mara mbili. Kwa njia hiyo utakuwa na uhakika na kiwango chake cha uvumilivu na kukomaa kwake kihisia,” Ahmad alisema.

Alisema kwamba hicho kinafaa kuwa kipimo si tu cha mapenzi bali pia kuangalia kama amekomaa katika kuwa na hofu ya Mungu na pia kuwa na moyo wa kuweza kusamehe.

“Kwa njia hiyo utakuwa na uhakika zaidi kama mwanamke unayetaka kumuoa ana hofu ya Mungu na moyo wa kusamehe. Mapenzi ya dhati ni lazima kusameheana,” aliongeza.

Hata hivyo wengine walitofautiana naye wakisema kwamba penzi linauma Zaidi kuliko kitu chochote na kujiweka katika mazingira ya kufumaniwa ni sawa sawa na kujihatarisha kimaisha kwani hasira inaweza ikamfunika mrembo macho na akaja kukufanyia kitu kibaya ambacho hata kitakusafirisha jongomeo.