Vera Sidika azungumza kuhusu kuolewa tena, afichua hali yake ya mahusiano

Mwanasholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika amepuuzilia mbali uwezekano wa yeye kuolewa tena.

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto wawili alidai kwamba ndoa ni mtego na kubainisha kwamba anapenda uhuru wake.

•Alisema licha ya kuwa na mpenzi anayeishi Nigeria, kwa sasa hayuko kwenye uhusiano wa dhati kwani hakuna majukumu.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika amepuuzilia mbali uwezekano wa yeye kuolewa tena.

Wakati akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram, mama huyo wa watoto wawili alidai kuwa ndoa ni mtego na kubainisha kwamba anapenda uhuru wake.

"Bado unaweza kupatia ndoa nafasi nyingine?" shabiki alimuuliza Jumatano asubuhi.

Huku akijibu, alisema “Kamwe siwezi, ni mtego. Napenda uhuru wangu.”

Aliambatanisha jibu lake na meme iliyosema kwamba hajali ni nani anapaswa kumwachilia aende mradi tu aendelee kuwa na furaha.

Alipoulizwa ikiwa yuko sawa na hali yake mpya, alisema kwamba anapitia wakati mzuri zaidi maishani mwake kwa kuwa anafurahia kuwa bila mchumba.

Huku akizungumzia ndoa yake iliyovunjika na mwimbaji Brown Mauzo, mwanasosholaiti huyo alifichua kuwa alianza kujitenga na uchumba huo takriban miezi minne kabla ya kuondoka rasmi.

"Kwangu, ilikuwa zaidi ya miezi 4 kabla ya kumalizika. Nilikuwa nimechoka kihisia, kimwili, kiakili,” alisema.

Aliongeza, "Kwa hivyo ilikuwa rahisi na uamuzi bora zaidi ambao nimewahi kufanya. Nilichagua mimi na nilitaka sana watoto wangu bora zaidi.”

Mama huyo wa watoto wawili alisema licha ya kuwa na mpenzi anayeishi Nigeria, kwa sasa hayuko kwenye uhusiano wa dhati kwani hakuna majukumu.

"Siko kwenye uhusiano wa dhati na sitaki ahadi. Kwa hivyo ndio, nipo single," alisema.

Mwishoni mwa Agosti mwaka jana, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"