Video ya Zari akishikana kimahaba na Diamond yamvunja moyo mumewe, adokeza matatizo katika ndoa

Wapenzi hao wawili kutoka Uganda walifunga pingu za maisha rasmi Oktoba mwaka jana

Muhtasari

•Huenda matatizo yalianza baada ya video inayomuonyesha Zari akitembea huku ameshikana mikono na ex wake Diamond Platnumz.

•Shakib Cham alijibu kwa njia isiyo ya moja kwa moja ambapo alidokeza kuwa hajafurahishwa na maendeleo ya hivi punde.

Zari Hassan, Diamond Platnumz, Shakib Cham
Image: INSTAGRAM//

Doa linaonekana kutokea katika ndoa changa ya wafanyabiashara wawili mashuhuri wa Uganda, Shakib Cham Lutaaya na mwanasosholaiti Zari Hassan.

Wapenzi hao wawili walifunga pingu za maisha rasmi Oktoba mwaka jana na wameonekana kufurahia nyakati nzuri kwenye ndoa yao katika miezi michache iliyopita hadi siku ya Alhamisi, Februari 22, ambapo Shakib alitoa vidokezo kuhusu matatizo fulani katika muungano wao unaozungumziwa sana.

Huenda matatizo yalianza baada ya video inayomuonyesha Zari Hassan akitembea huku akiwa ameshikana mikono na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Bosi huyo wa WCB alikuwa wa kwanza kuchapisha video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alimtambulisha mama huyo wa watoto wake wawili kama dada yake.

“Mimi na dada @zarithebosslady,” Diamond aliandika chini ya video hiyo.

Video hiyo iliyosambazwa siku ya Alhamisi jioni ilizua hisia mseto kutoka kwa wanamtandao tofauti ambao walitaka kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Zari alijibu, “aaai, nimekufa.”

Mume wa mwanasosholaiti huyo, Shakib Cham pia alijibu kwa njia yake mwenyewe isiyo ya moja kwa moja ambapo alidokeza kwamba hajafurahishwa na maendeleo ya hivi punde.

"Watu wenye nia safi wapate watu safi wenye nia safi," alichapisha kwenye instastories zake.

Pia alishiriki, "Mitandao ya kijamii inakufanya uvutie watu ambao unapaswa kuwaombea."

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alifuta picha nyingi zinazomuonyesha akiwa na Zari kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni pamoja na ile ya hivi punde aliyoshiriki mnamo siku ya wapendanao.

Zari na Shakib walirasimisha ndoa yao katika harusi ya faragha iliyofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwezi Oktoba mwaka jana. Wawili hao walikuwa wakichumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maelezo ya harusi hiyo yalikuwa yamefichwa sana lakini tulifanikiwa kupata baadhi ya picha na video za sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Picha hizo zilionyesha  Zari akiwa amevalia gauni la harusi refu jeupe huku mumewe Shakib akiwa amevalia suti ya kijivu na shati jeupe.

Wanafamilia wakiwemo watoto wa Zari; ; Pinto Tale, George Ssemwanga, Dido Ssemwanga Tiffah Dangote na Prince Nillan walikuwepo kwenye hafla hiyo. Tiffah alivalia gauni jeupe huku Nillan akiwa amevalia suti ya kijivu na shati jeupe sawa na bi na bwana harusi.

Wana wa Zari na aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga walionekana wamevalia suti nyeupe, shati jeupe na viatu vyeupe.

Wengi wa wageni waliokuwa wamealikwa kuhudhuria hafla hiyo ya faragha walionekana wamevaa mavazi meupe. Wanaume walikuwa na suti ya kijivu wakati wanawake walivaa gauni za rangi ya dhahabu.

Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu kwa mara ya kwanza katika harusi ya kidini ya Kiislamu (Nikah) mapema mwaka uliopita.