Rayvanny atuhumiwa kwa kumtapeli msanii mwenza milioni 7 kwa ahadi hewa ya kolabo

“…na pesa yangu wakachukua pasipo kuangalia kuwa mi ni kijana mdogo tena ninaepambania ndoto zangu kwa nguvu zote,” alisema kwa majonzi huku akiweka ushahidi wote.

Muhtasari

• "Kollabo hio nilipaswa kutafuta m.7 ambayo niliambiwa na ndugu director Elly Mzava ambaye yeye ndo atakae shoot video hio" alisimulia.

Rayvanny na Kayumba
Rayvanny na Kayumba
Image: Instagram

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amejipata katika hali tete baada ya kutuhumiwa kumtapeli msanii mwenza kwa jina Kayumba kisa kumuahidi kufanya kolabo naye.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kayumba kupitia Instagram ambapo alichapisha ushahidi wote kutoka mazungumzo hadi miamala, anadai Rayvanny pamoja na director wake kwa jina Mzava walimtaka kuwatumia shilingi milioni 7 za Kitanzania ambazo alituma lakini ujio wa kolabo ukawa kizungumkuti.

“Mnamo mwezi wa pili mwaka jana nilikuwa na project yangu ya album iliyoitwa ( fine tape ) humo ndani kuna collaboration kadhaa ikiwepo #shake niliomshirikisha ndugu yangu @rayvanny na kwenye collabo hio nilipaswa kutafuta m.7 ambayo niliambiwa na ndugu director Elly Mzava ambaye yeye ndo atakae shoot video hio. Nilimtafutia Mzava milioni 7 na nikamkabidhi ndani ya office za @nextlevelmusic_tz mbezi beach kwa kuamini nitapata kitu kizuri cha kuwapa fans wangu . lakini haikuwa hivyo, badala yake mizungusho ikaanza baada ya kuwapatia pesa na ile video tuliokubaliana haikufanyika mpka leo hii,” alisimulia.

 “…na pesa yangu wakachukua pasipo kuangalia kuwa mi ni kijana mdogo tena ninaepambania ndoto zangu kwa nguvu zote,” alisema kwa majonzi.

Baada ya kufichua uozo huu wa msanii Rayvanny, Kayumba pia alirudi akachapisha barua inayokisiwa kuandikwa na director huyo akikiri kwamba walichukua pesa zake na kukubali kumrudishia kiasi abacho kilimhusu lakini bado hakufanya hivyo.

Director Mzava alikiri kwa Kutoa kianzio cha Tsh mil 2 na Laki 9 ambapo kiasi kingine mil 2 aliahidi kutoa tarehe 4/5/2023 na Kiasi kingine kilichobaki mil 2 na Laki 1 aliahidi kumaliza Tarehe 14/05/2023 lakini Mpaka sasa Hazijalipwa.

Baadhi ya Picha kuhusiana na Barua pamoja na Charting zao walizochati, tayari zipo kwenye chapisho hili hapa chini katika ukurasa wa Kayumba.