Diamond athibitisha kuachwa na Zuchu, alilia maombi na sapoti anapopambana na ujane

Staa huyo ameomba sapoti na maombi akidokeza kuwa maisha yake bila mpenzi hayatakuwa rahisi.

Muhtasari

•Msanii Diamond Platnumz amethibitisha tangazo la awali la msanii wake Zuchu kwamba wao sio wapenzi tena.

•Taarifa hii ya Diamond ilikuja baada ya Zuchu kutangaza rasmi kuvunjika kwa uhusiano wao wa kimapenzi.

Diamond amethibitsha kuachwa na Zuchu

Staa wa Bongofleva, Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz amethibitisha tangazo la awali la msanii wake Zuchu kwamba wao sio wapenzi tena.

Katika taarifa yake Ijumaa jioni, bosi huyo wa WCB aliwataarifu mashabiki wake kwamba sasa yuko single kwa kuwa mpenzi wake amemuacha rasmi.

Aliendelea kuomba sapoti na maombi kutoka kwa mamilioni ya mashabiki wake akidokeza kwamba hatua inayofuata ya maisha yake bila mpenzi haitakuwa rahisi.

“Basi bwana wadau, ndio kama Mlivyosikia Matikiti Yamenidondokea….hivyo nahitaji sana Maombi Yenu, Huruma na Ukaribu wenu kipindi hiki cha Ujane wangu, ili kupata nguvu na faraja kwenye Kipindi Hiki Kigumu😭😭😭,” Diamond Platnumz alisema kupitia Instagram.

Staa huyo wa bongo fleva aliambatanisha taarifa yake na video iliyomuonyesha akiwa amesimama huku wimbo wake ‘Mapoz’ ukicheza nyuma.

Taarifa hii ya Diamond ilikuja baada ya Zuchu kutangaza rasmi kuvunjika kwa ghafla kwa uhusiano wake wa kimapenzi na bosi huyo wake.

Katika taarifa yake Ijumaa jioni, mwimbaji huyo mzaliwa wa Zanzibar alikiri kuwa kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi huyo wa WCB.

Hata hivyo, alifichua kuwa uhusiano huo uliozungumiwa sana kote barani Afrika umefikia kikomo akidokeza kuwa Diamond amemkosea heshima.

“HABARI FAMILIA .ILIBIDI KUPOST HII ILI KUFUTA DHAMIRI YANGU. KUANZIA LEO HII MIMI NA NASIBU (DIAMOND) HATUKO PAMOJA,” Zuchu alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliongeza, “NAJUA HILI LIMEKUWA JAMBO LETU LAKINI AS HARD AS IT IS KUMUACHA MTU UNAEMPENDA HII NAOMBA MUNGU IWE YA MWISHO NA NIANZE MAISHA MAPYA. MAPENZI NI HESHIMA KWA BAHATI MBAYA SANA HIKO KIMEKOSEKANA KWETU.”

Licha ya kusambaratika kwa uhusiano wao wa kimapenzi, Zuchu hata hivyo aliweka wazi kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja katika WCB.

Binti huyo wa Khadija Kopa alitangaza kuwa sasa yuko single akibainisha wazi kuwa yuko tayari kwa sura mpya ya maisha yake kama mtu huru.

“NAMTAKIA YEYE NA FAMILIA YAKE KILA LA KHERI KABISA .TUMEISHI VIZURI LAKINI NADHANI HII SIO RIZKI .MWAKA HUU NIMEJIFUNZA KUSEMA HAPANA KWA KILA KITU KISICHONIPA FURAHA AMA BAADA YA KUSEMA HAYA NAONA KABNYE MASHAURI YA KUFURAHIA NA KUFURAHIA MPAKA . . KWA SASA KAZI IENDELEE NA MIMI NIKO SINGLE ���.,” Zuchu alisema.

Tangazo hili lilikuja saa chache baada ya Diamond Platnumz kuonekana akiwa ameshikana mikono kimahaba na mzazi mwenzake Zari Hassan.