Aliyekuwa mpiga picha wa Diamond avunja kimya baada ya video za uchi kuanikwa mtandaoni

Pia ameomba radhi kwa watu wote walioguswa na sakata hilo ambalo limekuwa likiendelea.

Muhtasari

•Mange Kimambi alidai kumiliki video za uchi za Lukamba na hata akashare screenshot ya klipu aliyodai kuwa nayo huku akitishia kuzianika zote kupitia app yake.

•Mpiga picha huyo aliwataka watu kuacha kumchafulia jina na akaahidi kusema ukweli wote punde baada ya mfungo wa Ramadhani.

katika picha ya maktaba.
Lukamba na Diamond katika picha ya maktaba.
Image: HISANI

Aliyekuwa mpiga picha rasmi wa staa wa bongo Diamond Platnumz, Lukamba amevunja ukimya kufuatia vitisho vya kuanika video zake za uchi.

Siku ya Ijumaa, mwanablogu wa Tanzania Mange Kimambi, ambaye kwa sasa anaishi Marekani, alidai kumiliki video za uchi za Lukamba na hata akashare screenshot ya klipu aliyodai kuwa nayo huku akitishia kuzianika zote kupitia app yake.

Huku akijibu, Lukamba ambaye aliondoka Wasafi mwaka 2022, alikiri kuwa mwanaume ambaye alionyeshwa kwenye screenshot ya video  iliyoshirikiwa kwenye Instagram kweli ni yeye akiwa ndani ya nyumba ambayo alikuwa akiishi na mpenzi wake wa zamani. Hata hivyo, alibainisha kuwa video hizo ni za zamani, na akabainisha kuwa tayari ameachana na mwanamke ambaye alikuwa naye.

“Asalaam alykum, kwanza kabisa niseme Alhamdulilah kwa kila kitu ambacho kibaya au kizuri. Napigiwa simu sana na kutumiwa screenshot zikinionesha nipo chumbani hapo ni nyumbani tulipo kuwa tunaishi mm na Ex wangu na hizo clip au video anazo huyo Ex wangu ni za muda,” Lukamba alisema.

Aliongeza, “Kuachana na mtu sio vita … yameongelewa maneno mengi ya uongo kwenye jamiii nimekaaa kimyaaa ila haitoshi mmekuja na video, mkisema watu wote Lukamba mkorofi lukamba hana adabu kwa wanawake. Hata kama kuforce ustar this is too much ������ una mtoto wa kiume kumbuka wewe ni mama.”

Mpiga picha huyo aliwataka watu kuacha kumchafulia jina na akaahidi kusema ukweli wote punde baada ya mfungo wa Ramadhani.

Pia ametoa pole kwa watu wote walioguswa na sakata hilo ambalo limekuwa likiendelea.

”Naombeni nifunge swaumu yangu kwa amani .. nitaongea ukweli Ramadhani ikiisha. Niwaombe radhi wote walio kwazika hii ni fitna tu ndugu zangu binadamu wakiamua kufanya ubaya hawaangaii pa kukupiga ila niwakumbushe mimi sio myongeee ������ TUTAPAMBANA,” alisema.

Lukamba alitengana na Diamond Platnumz katikati ya mwaka wa 2022 na kuanzisha kampuni yake inayoitwa Imagix Media. Kampuni hiyo inajishughulisha na maudhui yanayohusiana na video - harusi, picha za picha, makala na filamu.