"Mimi ni baba mzuri" Samidoh azungumzia uhusiano na watoto wake na Karen Nyamu na Edday Nderitu

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amejigamba kuhusu uwezo wake kama baba.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo ambaye katika siku za nyuma amehusishwa katika drama nyingi alisema anawajibika sana na watoto wake.

•Alisema huwa anajaribu kuwaeleza wanawe kuhusu mambo yanayozungumziwa hadharani, na kuwaonya kuhusu mambo ya kutarajia.

Samidoh
Samidoh
Image: HISANI

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amejigamba kuhusu uwezo wake kama baba.

Akizungumza katika mahojiano na SPM Buzz, mwimbaji huyo ambaye katika siku za nyuma amewahi kuhusishwa katika drama nyingi alisema anawajibika sana na watoto wake.

Samidoh ana watoto watatu na mke wake wa kwanza Edday Nderitu ambaye alihamia Marekani pamoja nao, na wengine wawili na seneta Karen Nyamu.

"Huenda nisiwe mambo mengi, lakini mimi ni baba mzuri," Samidoh alisema.

Aliongeza, “Siku zote nipo kwa ajili ya watoto wangu. Siku zote nipo kwa ajili yao. Inapofikia muda nao, linapokuja suala la usaidizi wa kifedha, mimi huwa nipo kwa ajili yao kila wakati. Wote."

Mwanamuziki huyo mahiri alivishutumu vyombo vya habari kwa kuzidisha mambo na kumnukuu vibaya, akisema kwamba yeye na familia yake hawana matatizo.

Alisema huwa anajaribu sana kuwaeleza watoto wake kuhusu mambo yanayozungumziwa hadharani, na kuwaonya kuhusu mambo ya kutarajia.

"Huwa nazungumza na binti yangu, kwa sababu yeye ndiye mkubwa kuliko wale wengine. Even the others, nikipata nafasi nawaongelesha hapa na pale.

Huwa nawaambia this is not it kwa sababu kuna wakati mwingine utakaambiwe ulikuwa unataka kupindua serikali, na hiyo ata haikuwa akilini mwako. Vyombo vya habari pia vinaharibu mambo,” alisema Samidoh.

Mapema mwaka huu,  mwimbaji huyo wa Mugithi alifunga safari hadi Marekani kuwatembelea watoto wake watatu na aliyekuwa mkewe, Edday Nderitu. 

 

Mke wa msanii huyo wa miaka mingi, Edday Nderitu kwa sasa anaishi Marekani pamoja na watoto wao.  Aliondoka nchini mapema mwaka jana na anaonekana tayari kutulia huko vizuri huku watoto wakiwa wameanza shule huko.

Mwezi Julai mwaka jana, Bi Edday Nderitu aliweka wazi kwamba alimuacha mumewe ili awe na mwanamke ambaye alionekana kumtaka zaidi.

"Wacha nifafanue mambo machache ambayo yalishirikiwa mtandaoni na sio sahihi. Siko kwenye ndoa ya wake wengi, kama ilivyoelezwa nilimuacha mume kwa yeyote aliyemhitaji zaidi,” Edday alisema kupitia Facebook.

Aliongeza, "Nilifanya uamuzi wa kujiondoa mimi na watoto wangu kutoka kwa mazingira hayo yenye sumu, haswa binti yangu kijana ambaye kwa bahati mbaya anapokea moja kwa moja tabia isiyoaminika iliyoonyeshwa."

Samidoh ana watoto wengine wawili na mpenzi wake Karen Nyamu ambao wanaendelea kule pamoja.