Maoni mseto Pasta akimdhalilisha msichana kanisani kwa kudai ushuhuda wake ni feki (video)

Msichana huyo alisimama utoa ushuhuda wake jinsi alifuzu na digrii katika sheria lakini pasta akamwambia kwamba hakuna kozi kama hiyo huku pia akisema mhitimu wa sheria hazungumzi jinsi mrembo alivyozungumza.

Muhtasari

• Mwanamke huyo, Anyim Vera, ambaye alidai kuwa alihitimu na "Bsc katika Sheria" kutoka Chuo Kikuu Huria cha Kitaifa cha Nigeria, alikatishwa na Enenche, ambaye alimshutumu kwa kusema uwongo.

• Alimwambia haonekani kama mhitimu wa Sheria, akienda kwa jinsi alivyozungumza. Pia alimwambia kwamba hakuna kitu kama “Bsc in Law” na akamtaka aondoke kwenye madhabahu.

Mchungaji apuuzilia mbali ushuhuda
Mchungaji apuuzilia mbali ushuhuda
Image: Screengrab

Watumizi wa mitandao ya kijamii haswa kutoka nchini Nigeria wametoa wito kwa Mchungaji mmoja baada ya video kuibuka ikionyesha jinsi alimdhalilisha msichana ambaye alikuwa anatoa ushuhuda kwenye madhabahu ya kanisa lake.

Mchungaji huyo aliyetambuliwa kwa jina Paul Enenche wa kanisa la Dunamis Internationa Gospel Centre aliburuzwa mitandaoni na watu wakimtaka kuomba msamaha kwa muumini wa kanisa lake ambaye aliaibishwa hadharani na kushutumiwa kwa kukosa uaminifu wakati wa kikao cha kutoa ushahidi.

Video ambayo ilisambaa siku ya Jumapili ilimuonyesha Enenche akihoji uaminifu wa ushuhuda wa mwanamke huyo katika kanisa lake huko Abuja.

Mwanamke huyo, Anyim Vera, ambaye alidai kuwa alihitimu na "Bsc katika Sheria" kutoka Chuo Kikuu Huria cha Kitaifa cha Nigeria, alikatishwa na Enenche, ambaye alimshutumu kwa kusema uwongo.

Alimwambia haonekani kama mhitimu wa Sheria, akienda kwa jinsi alivyozungumza. Pia alimwambia kwamba hakuna kitu kama “Bsc in Law” na akamtaka aondoke kwenye madhabahu.

Kufuatia tukio hilo, wanamtandao walichakura na kuibua ukurasa wa Facebook wa mwanamke huyo na picha zinazothibitisha kuwa alihitimu kutoka chuo hicho.

Pia, orodha ya wahitimu walioshiriki katika kusanyiko la Jumamosi, Aprili 13, ilitia ndani jina la mrembo huyo. Aliorodheshwa kuwa amehitimu na Sheria ya LLB.

Video hiyo imezua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakimtaka Enenche kuomba radhi kwa kitendo chake, huku wengine wakitetea msimamo wake.

Wengine wanasema kwamba ukosefu wa ufasaha wa mwanamke unaweza kusababisha kutokuelewana, wakati wengine wanaamini kwamba mbinu ya Enenche ilikuwa kali.

Mtumiaji wa X, Soulmedika, aliandika, "Kitu pekee ambacho Mchungaji Paul Enenche anahitaji kufanya kwa mwanamke huyo ni kuomba msamaha na inapaswa kuwa nyingi! Visingizio vyote vya ‘si kosa la Mchungaji, mwanamke alipaswa kutaja jina la shahada yake’ ni lelemama! Ndiyo, wote wanapaswa kuacha kutenda kama Ukristo ni dhehebu!”

iredafeowolabi aliandika, “Kuwa mhitimu wa sheria haimaanishi lazima uwe na ufasaha. Alipitia programu ili kuwa mtu bora katika njia anayofikiria na kuchakata habari.”

Naturalboifilmz aliandika, "Kuna njia nzuri zaidi ya kushughulikia hali hii, hata kama alisema uwongo. Mtazamo wa mchungaji ulikuwa wa kujishusha kupita kiasi. Ni haki sana.”

"Kitu kimoja nilimwambia mama yangu baada ya kuona video kwenye IG. Hajui Kiingereza sana, lakini unaweza kujua kutokana na mshtuko usoni mwake kwamba alimaanisha kile alichosema ingawa hakuweza kutetea," FavourDiamen aliongeza.

Tazama video hiyo hapa chini;

 

AdvebturousAlec aliandika, "Mchungaji hajakosea na mwanamke pia hajakosea, alifanya makosa baada ya kutambua kwangu. There's nothing like a BSc in Law but LLB in Law, ambayo ni Shahada ya Sheria. Paul Enenche alimjibu kulingana na jibu lake, 'Bsc' sio kwa sababu aliona uthibitisho halali wa ushahidi. Alijiletea mwenyewe, lakini kama mchungaji, angependa kudumisha amani.”