“Ulituletea furaha nyingi” Samidoh, Edday Nderitu waungana kumsherehekea mtoto wao

Edday na Samidoh wana watoto watatu pamoja, binti wawili na wa kiume.

Muhtasari

•Wawili hao ambao hawaishi pamoja tena walichukua muda kuandika jumbe nzuri kwa mtoto wao kuthibitisha upendo wao mkubwa kwake.

•Edday alizungumza kuhusu athari nzuri ambayo kuzaliwa kwa mvulana huyo wa miaka minane ilikuwa nayo katika maisha yao.

wamemsherehekea mtoto wao Samidoh Jr
Samidoh na Edday Nderitu wamemsherehekea mtoto wao Samidoh Jr
Image: HISANI

Wazazi wenza Samidoh na Edday Nderitu walimsherehekea mtoto wao wa pili Samidoh Jr alipoadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya nane mnamo Jumatano, Mei 30.

Samidoh, Edday Nderitu waungana kumsherehekea mtoto wao

Samidoh alimtakia mwanawe siku njema ya kuzaliwa na kukiri jinsi alivyojivunia kumuona akikua.

"Kukuona ukikua kuwa mtu wa ajabu leo imekuwa furaha kuu ya maisha yangu. Hapa ni kwa miaka mingi ya furaha, upendo, na mafanikio! Kheri ya siku ya kuzaliwa mwanangu!!,” Samidoh alimwandikia mwanawe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya kijana huyo.

Kwa upande wake, Edday Nderitu alizungumza kuhusu athari nzuri ambayo kuzaliwa kwa mvulana huyo wa miaka minane ilikuwa nayo katika maisha yao. Pia alionyesha upendo wake mwingi kwake na kuthibitisha jinsi anajivunia kuwa mama yake.

"Miaka minane iliyopita, ulileta furaha na upendo mwingi katika maisha yetu, na kila siku tangu wakati huo imekuwa zawadi. Akili yako ya udadisi, moyo wako mzuri, na roho yako ya ujanja hunifanya nijivunie kuwa mzazi wako,” Edday aliandika kwenye Instagram.

Aliongeza, "Hapa ni kwa miaka mingi zaidi ya kicheko, kujifunza, na kutengeneza kumbukumbu pamoja! Siku yako iwe nzuri na ya ajabu kama wewe! Ninakupenda zaidi ya maneno yanaweza kusema! HERI YA SIKU YA 8 YA KUZALIWA MVULANA WANGU MZURI❤️."

Edday na Samidoh wana watoto watatu pamoja, binti wawili na wa kiume. Wazazi hao wawili hata hivyo hawaishi tena pamoja kwani Edday alihamia Marekani mwaka jana kufuatia drama nyingi zilizoibuka katika ndoa yao ya miaka mingi.

Mapema mwaka huu,  mwimbaji huyo wa Mugithi alifunga safari hadi Marekani kuwatembelea watoto wake watatu na mke huyo wake wa kwanza. 

Mke wa msanii huyo wa miaka mingi, Edday Nderitu kwa sasa anaishi Marekani pamoja na watoto wao.  Aliondoka nchini mapema mwaka jana na anaonekana tayari kutulia huko vizuri huku watoto wakiwa wameanza shule huko.

Mwezi Julai mwaka jana, Bi Edday Nderitu aliweka wazi kwamba alimuacha mumewe ili awe na mwanamke ambaye alionekana kumtaka zaidi.

"Wacha nifafanue mambo machache ambayo yalishirikiwa mtandaoni na sio sahihi. Siko kwenye ndoa ya wake wengi, kama ilivyoelezwa nilimuacha mume kwa yeyote aliyemhitaji zaidi,” Edday alisema kupitia Facebook.

Aliongeza, "Nilifanya uamuzi wa kujiondoa mimi na watoto wangu kutoka kwa mazingira hayo yenye sumu, haswa binti yangu kijana ambaye kwa bahati mbaya anapokea moja kwa moja tabia isiyoaminika iliyoonyeshwa."