Mbosso akiri kupata mtoto na aliyekuwa mke wa kakake Alikiba

"Ndiyo, nina mtoto na yule mwanamke ambaye awali aliolewa na Abdu Kiba," Mbosso alisema

Muhtasari

•Ninajaribu kadiri niwezavyo kuwa na uhusiano mzuri naye lakini wakati mwingine ni ngumu, tuko hapa na tunashughulika na mtoto.

•Ni swala ambalo lilileta maswala mengi sana kwenye mahusiano yetu maana nilikuwa muwazi sana kwake lakini alikuwa hajaniambia mambo mengi

Mbosso
Image: instagram

Mwimbaji wa Tanzania Mbosso amekiri kupata mtoto na mwanamke ambaye aliwahi kuolewa na mdogo wa Alikiba, Abdukiba.

Muimbaji huyo wa WCB alifunguka hayo alipokuwa akihojiwa na Wasafi FM hivi karibuni ambapo alikiri kuhusika na mwanadada huyo hadi kufikia hatua ya kuwa na mtoto naye.

"Ndiyo, nina mtoto na yule mwanamke ambaye awali aliolewa na Abdu Kiba," Mbosso alisema.

Kulingana na Mbosso, hakuwahi kufahamu uhusika wowote kati ya mama yake mzazi na ndugu huyo wa Ali Kiba.

Mwimbaji huyo aliendelea kumlaumu mwanadada huyo akisema aliiweka ndoa yake na Abdukiba kuwa siri kwa muda mrefu hivi kwamba yeye (Mbosso) alikuja kujifunza mengi baadaye.

"Ni swala ambalo lilileta maswala mengi sana kwenye mahusiano yetu maana nilikuwa muwazi sana kwake lakini alikuwa hajaniambia mambo mengi. Nilipokuja kugundua kuwa ni mke wa zamani wa Abdu Kiba, nilikuwa nimechelewa." Alieleza.

Ingawa anajilaumu kwa kutochukua muda kumjua mpenzi wake wa wakati huo, Mbosso anasema kilichobaki ni wao kumlea mtoto waliyemzaa pamoja.

"Ninajaribu kadiri niwezavyo kuwa na uhusiano mzuri naye lakini wakati mwingine ni ngumu, tuko hapa na tunashughulika na mtoto.

Kadhalika, Mbosso alikiri kuwa na uhusiano mbaya na mwanadada huyo akisema hawakuzungumza lakini wanagombana karibu kila mara wanapozungumza.

"Tunazungumza lakini tunagombana sana. Kuna wakati tunatupiana cheche za maneno na hatuwezi kumaliza mwezi bila kugombana.