Simon Pegg akabiiwa marufuku ya pili ya uendeshaji gari kwa kasi

Nyota huyo maarufu wa Mission Impossible angoja hukumu yake Juni 24

Muhtasari

• Alikamatwa akiendesha kwa kasi ya 20mp/h mjini London. 

•Amejipata matatani baada ya kukiri kosa jingine la mwendo wa kasi mjini Hackney Oktoba 24 mwaka jana

Nyota wa sinema Mission Impossible Simon Pegg
Image: HISANI

Nyota wa sinema ya Mission Impossible Simon Pegg anakabiliwa na marufuku yake ya pili ya kuendesha gari ndani ya miaka mitatu baada ya kukamatwa akiendesha kwa kasi ya 20mp/h katika moja ya maeneo ya London.

Muigizaji na mwandishi aliyeshinda tuzo za mcheshi bora, 54, alitumikia marufuku ya miezi sita mnamo 2021 baada ya kupata alama 13 za adhabu kwenye leseni yake kwa makosa manne ya mwendo kasi.

Wakati huo, wakili wake aliiambia mahakama ya Wimbledon kuwa, "Pegg anajutia sana makosa na kupigwa marufuku kungemsababishia matatizo zaidi".

Nyota huyo amejipata matatani ghaya baada ya kukiri kosa zaidi la mwendo kasi mjini Hackney Oktoba 24 mwaka jana. Alikubali hatia kupitia utaratibu mmoja wa haki katika mahakama ya Lavender Hill mwezi uliopita, na sasa anakabiliwa na marufuku nyingine inayoweza kutokea.

Nyaraka za mahakama zinaonyesha Pegg alikuwa nyuma ya gurudumu la Mercedes AMG katika Barabara ya Homerton huko Hackney Wick saa 10.54 asubuhi .Inasemekana kuwa, gari lilikuwa likiendakwa kasi ya 36mp/h katika eneo la kasi ya 20mp/h.

Pegg vilevile, nyota maarufu wa filamu ya Shaun of the Dead, aliandikiwa na polisi nyumbani kwake huko Hertfordshire mwezi Aprili makosa haya ambayo alithibitisha kuwa alikuwa akiendesha gari wakati wa tukio hilo.

Aliwasilisha ombi la hatia kwa maandishi bila kupunguzwa ambayo afisa wa mahakama alithibitisha. Hakimu alisikiliza kesi dhidi ya Pegg kwa faragha Mei 20.

Hukumu imeahirishwa hadi kusikilizwa kwa kesi mnamo Juni 24 kuzingatia kunyimwa haki ya kuendesha gari. Baada ya kusikilizwa kwa mahakama ya 2021, Pegg alitozwa faini ya £660 na kuamuru kulipa gharama ya £85.