Msanii Jay Melody achoka kuitwa mbilikimo, akiri kuwa mfupi na kutoa onyo kwa wanaomcheka

“Jamani wenangu ni kweli mimi si mrefu. Nimechoka kila nikikutana na watu eti kumbe ni kadogo hivi. Ndio, mimi ni mfupi, kwa hiyo ieleweke basi maana imekuwa kama masimango sasa,” Jay Melody alisema.

Muhtasari

• Melody alikiri kwamba yeye ni mfupi na kusema kwamba alilazimika kufanya hivyo ili kuweka kikomo kwa wale wanaomcheka baada ya kukutana, kwani imezidi na kuwa masimango sasa.

Jay Melody.
Jay Melody.
Image: Screengrab

Mwimbaji wa Bongo Fleva, Jay Melody amewafokea vikali baadhi ya mashabiki wake ambao humcheka na kumsimanga kwa ufupi wake pindi wanapokutana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jay Melody alichapisha ujumbe wa kukiri kuhusu ufupi wake na kusema kwamba baadhi ya mashabiki ambao wanamsikia kwenye miziki na pengine kumtazama kweney video wanadhani ni mrefu jambo ambalo huwa kinyume wanapomkuta ana kwa ana na wengine hata kuanza kumcheka.

Melody alikiri kwamba yeye ni mfupi na kusema kwamba alilazimika kufanya hivyo ili kuweka kikomo kwa wale wanaomcheka baada ya kukutana, kwani imezidi na kuwa masimango sasa.

“Jamani wenangu ni kweli mimi si mrefu. Nimechoka kila nikikutana na watu eti kumbe ni kadogo hivi. Ndio, mimi ni mfupi, kwa hiyo ieleweke basi maana imekuwa kama masimango sasa,” Jay Melody alimaliza kwa emoji ya kucheka.

Msanii huyo ambaye alipaa kweye anga za muzingi pendwa wa Bongo Fleva mapema mwaka 2021 kwa sasa anazidi kutamba na albamu yake ya Therapy.