Mama Dangote afichua DJ wa Diamond, Romy Jons alinyonya ziwa lake japo hakumzaa

Pia alisema kwamba wimbo Diamond na Mr Blue na Jay Melody unamkumbusha enzi za zamani akicheza disco na mamake Mr Blue.

Muhtasari

• " Romy kanyonya ziwa langu ujue. Mamake anasafiri nabaki na yeye, nakuwa na Romy na Naseeb" alisema.

Image: INSTAGRAM// MAMA DANGOTE

Mamake Diamond Platnumz amefichua uhusiano uliopo kati yake na Romy Jons, DJ rasmi wa Diamond ambaye aghalabu wengi wanamjua kama mwanawe wa kumzaa na ndugu wa toka nitoke wa Diamond na Esma.

Katika mahojiano ya Refresh kwenye Wasafi siku chache zilizopita, Mama Dangote alifunguka ukweli kwamba Romy Jons si mwanawe wa kumzaa lakini amechangia pakubwa katika kumlea na hata kipindi akiwa mdogo alikuwa anamnyonyesha yeye.

Alisema kwamba kinachowafanya wengi kuchanganyikiwa na dhana kwamba Romy Jons ni mwanawe wa kumzaa ni kutokana na jinsi alivyomlea akiwa mdogo kipindi hicho naye pia akiwa na Diamond.

Kwa hiyo, aliwalea wote kwa zamu moja kama mapacha.

Lakini ilitokeaje mpaka Mama Dangote akawa anamlea na kumnyonyesha Romy Jons licha ya kutomzaa yeye, na vipi kuhusu wazazi wake?

“Mamake Romy Jons alikuwa anafanya biashara. Alikuwa anasafiri sana, sasa mimi nikawa ndio namlea Romy Jones. Nimewalea yeye na Naseeb [Diamond] maanake wamekua kama mapacha. Romy kanyonya ziwa langu ujue. Mamake anasafiri nabaki na yeye, nakuwa na Romy na Naseeb. Yaani Romy ananipenda hatari,” Mama Dangote alisema kwa kujitapa.

Pia alisema kwamba wimbo Diamond na Mr Blue na Jay Melody unamkumbusha enzi za zamani akicheza disco na mamake Mr Blue.