Mulamwah na Carrol Sonie wamsherehekea binti yao, Keilah

Mpenzi we Mulamwah, Ruth K pia aliandika ujumbe mzuri wa heri ya siku ya kuzaliwa kwa msichana huyo.

Muhtasari

•Katika ujumbe wake, Carrol Sonie alionyesha fahari na upendo wake kwa bintiye na kumtia moyo kuhusu jinsi ya kukabiliana na maisha.

•Mulamwah kwa upande wake alichapisha picha nzuri za bintiye ili kumsherehekea na akamtambua kama malkia.

Image: INSTAGRAM//

Binti ya wapenzi wa zamani Mulamwah na Caroline Muthoni, Keilah Oyando, anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya tatu hivi leo, Septemba 17, 2024.

Wazazi wote wawili wametumia fursa hiyo kumsherehekea malkia huyo mdogo kwa jumbe nzuri na kumtakia kila la heri anapoendelea kuwa mkubwa.

Katika ujumbe wake, muigizaji Carrol Sonie alionyesha fahari na upendo wake kwa bintiye na kumtia moyo kuhusu jinsi ya kukabiliana na maisha.

“Heri ya siku ya kuzaliwa maitu🎉👸 @keilah_khloe_kk . Nataka ukue ukijua kuwa kila kitu kinawezekana mpenzi,” Sonie alimwandikia bintiye kupitia Instagram.

Aliongeza, “Ninajivunia wewe mama. Ngwendete ta bomu (Nakupenda kama bomu)❤️”

Mchekeshaji Mulamwah kwa upande wake alichapisha picha nzuri za bintiye ili kumsherehekea na akamtambua kama malkia.

"Ni siku ya kuzaliwa ya 3 ya malkia," Mulamwah aliandika.

Pia alizungumza kuhusu azimio lake kubwa la kutengeneza kumbukumbu nzuri na msichana huyo wa miaka mitatu.

"Wow , muda unapepea🎂🎂 tayari ni miaka 3 kwa malkia ❤️❤️ nisaidieni kumtakia KEILAH siku njema ya kuzaliwa 3 . Kwa miaka mingi zaidi ya afya njema na mafanikio binti yangu , kamum ana furaha ❤️❤️ siwezi kusubiri kuunda kumbukumbu nyingi pamoja,” aliongeza.

Mpenzi wa sasa wa Mulamwah, Ruth K pia aliandika ujumbe mzuri wa heri ya siku ya kuzaliwa kwa msichana huyo anapoadhimisha siku yake maalum.

"Happy birthday babygirl," Ruth alijibu post ya mpenzi wake.

Keilah alizaliwa mnamo Septemba 17, 2021, miezi michache tu kabla ya wazazi wake mashuhuri kutangaza mwisho wa mahusiano yao.