Akothee adaiwa 'kuiba' mume wa mwanadada wa Mombasa, ajibu jinsi alivyokutana na mpenziwe

Mama huyo wa watoto watano alidaiwa 'kuiba' mume wa mwanadada wa Mombasa.

Muhtasari

•Akothee amefichua kuwa alikutana na mzungu huyo katika Ziwa Zug, nchini Uswizi mnamo July 16, 2022.

•Alilazimika kufafanua kuhusu jinsi alivyokutana na mzungu huyo baada ya kushtumiwa kwa kuiba mpenzi wa mtu.

'Omondi' na Akothee
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu Esther Akoth almaarufu Akothee amesimulia hadithi ya jinsi alivyokutana na mchumba wake wa sasa 'Omondi.'

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, amefichua kuwa alikutana na mzungu huyo katika Ziwa Zug, nchini Uswizi mnamo July 16, 2022.

Mama huyo wa watoto watano amefichua kuwa walijipata na mchumba wake katika na  kikao cha kibiashara kilichokuwa kimeandaliwa na rafiki yao ambapo Omosh alichukua simu yake na kusave namba yake kama 'Mume Wangu'.

"Tulienda kuogelea kwenye ziwa Zug na baadaye tukarudi nyumbani. Kitu cha kuchekesha kilitokea, sisi sote tulikuwa tumevutiana sana, sikuwa namba yake lakini alikuwa na yangu, kwani alisave yake kwenye simu yangu na kupiga simu yake."

Kisha baadae akampigia simu rafiki yake na kusema anataka kuongea na mimi kwenye video call, tukazungumza, kisha akaniuliza,  nimpigie na simu yangu, na nikamwambia kuwa sina namba yake," alisimulia.

Akothee alisema alishtuka sana baada ya kugundua kuwa mzungu huyo alijisave kama 'Mume wangu' kwenye simu yake.

Alisema baada ya wao kufahamiana ,Omosh alianza kumwonyesha mapenzi makubwa na kumdekeza kama msichana mdogo, jambo ambalo hakuwahi kushuhudia na mwanamume yeyote ambaye aliwahi kuchumbiana naye hapo awali.

"Tulienda kupimwa UKIMWI kabla ya chochote. Na baada ya wiki tatu, ainitambulisha kwa familia na marafiki zake, Omosh ana familia nzuri, nilikwama hapo"

Mwimbaji huyo alisema kwamba hakuamini na alifikiri alikuwa akiota siku ambayo mpenzi wake alimchumbia na kumvisha pete ya uchumba.

Alisema mwanzoni hakupanga kuweka mahusiano yake na mzungu huyo hadharani lakini aligundua hangeweza kuficha kwa muda mrefu kwa  kuwa yeye ni mtu maarufu  na hakutaka watu wachanganye mpenziwe na watu wengine.

"Nakupenda @misteromosh wangu. Mungu adumishe MUUNGANO wetu. Nitaoa rafiki yangu wa dhati. Nilikubali ndoa miezi mitatu iliyopita," alisema.

Mama huyo wa watoto watano alilazimika kufafanua kuhusu jinsi alivyokutana na mzungu huyo baada ya kushtumiwa kwa kuiba mpenzi wa mtu.

Ripoti zilizoenea mtandaoni zilidai kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alinyakua mume wa mwanamke mmoja anayeishi Mombasa ambaye alikuwa akipanga kuanzisha naye biashara humu nchini Kenya.

Akothee anadaiwa 'kumuiba' Omosh kutoka kwa mwanamke huyo baada ya kuwaunganisha kwa ajili ya biashara, madai ambayo mwanamuziki huyo sasa amekanusha.