Akothee aeleza kwa nini hatachumbiana na mwanamume mdogo tena baada ya kutengana na Nelly Oaks

Akothee aliweka wazi kuwa anataka kudekezwa kama mtoto katika mahusiano yake yajayo.

Muhtasari

โ€ขMama huyo wa watoto watano amefanya maazimio ya kuchumbiana tu na wanaume waliomzidi umri katika hatua yake mpya.

โ€ขTangazo hili takriban mwezi mmoja baada yake kutangaza kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks.

Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee ametimiza umri wa miaka 42.

Kati ya maazimio ambayo mama huyo wa watoto watano amefanya katika hatua yake mpya ni kuchumbiana tu na wanaume waliomzidi umri.

Akothee alitoa kauli hiyo  Jumanne kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka wazi kuwa anataka kudekezwa kama mtoto katika mahusiano yake yajayo.

"Katika maisha yangu yajayo, sitaenda kuchumbiana na mtu yeyote mdogo kuliko mimi, nataka kuwa mtoto ndani ya nyumba . Unanihisi ๐Ÿ’‹๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ. Inahisi vizuri kutunzwa kama mwanamke ๐Ÿ‘ ," Akothee alisema.

Msanii huyo  aliweka umri wa chini kabisa wa mwanaume ambaye yupo tayari kuchumbiana naye kuwa miaka 40+.

"Isipokuwa awemdogo na ubongo wa miaka 50, hapo tunaweza kufaana,"  Alisema.

Tangazo hili takriban mwezi mmoja baada yake kutangaza kutengana na aliyekuwa mpenzi wake kwa miaka minne, Nelly Oaks.

Mwezi uliopita mwanamuziki huyo alitangaza kwamba yupo single huku akifichua kuwa alitengana na Oaks mwezi Desemba 2021.

"Mapenzi ni matamu, na ni matamu unapopatana na mtu anayefaa, mapenzi yatakupata kwa njia moja au nyingine,lakini cha muhimu ni nguvu ambayo mnaleeta wenye uhusiano wenu wa mapenzi.. Mnapoachana kila mtu huwa ameumia kutoka kwenye uhusiano huo, naweza kusema nilitoka kwenye uhusiano wangu na Nelly Oaks Desemba," Alisema katika mahojiano na Presenter Ali.

Oaks ambaye awali alikuwa meneja wa Akothee kabla ya kugeuka kuwa mpenzi anaaminika kuwa mdogo kumliko takriban miaka 10.

Mwanamuziki huyo alidokeza kuvunjika kwa mahusiano yao Aprili mwaka huu wakati ambapo aliwashauri watu kutochukulia mahusiano kwa makini.

""Unakumbuka nilipowaambia nimechukuliwa? Kusema kweli hadi kifo kinatutenganisha tu amefunga virago na kuondoka! Mimi niko single tena jamani... barabara ya mahusiano huwa inajengwa kila wakati," Aliandika kwenye Instagram.

Wawili hao walijitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2018 baada ya kufanya kazi pamoja kwa muda.