Baha afunguka uhusiano na Georgina baada ya video zake chafu kusambazwa, aapa kumshtaki aliyehusika

"Yuko shwari, hata niko naye," Baha alisema.

Muhtasari

•Wapenzi hao waligeuka kuwa gumzo mitandaoni baada ya video zinazodaiwa kuwa za Bi Georgina akicheza akiwa uchi kuvujishwa.

• Baha alifichua kwamba wanajiandaa kumshtaki mhusika kwa aibu aliyomletea mpenziwe. 

Muigizaji Tyler Mbaya na mpenzi wake Georgina Njenga
Image: INSTAGRAM// TYLER MBAYA

Muigizaji Tyler Kamau Mbaya almaarufu Baha kutokana na kipindi 'Machachari' amemhakikishia mpenzi wake Georgina Njenga kuhusu mapenzi yake makubwa kwake licha ya video yake chafu ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi majuzi, wapenzi hao waligeuka kuwa gumzo mitandaoni baada ya video zinazodaiwa kuwa za Bi Georgina akicheza akiwa uchi kuvujishwa.

Baha hata hivyo ameweka wazi kuwa tukio hilo halijatikisa mahusiano yake hata na kufichua kwamba bado wako pamoja.

"Mapenzi yapo, mapenzi hayawezi tingishwa na sio hoja kwa hili," alisema katika mahojiano na kituo moja cha redio cha hapa nchini.

Baha alifichua kuwa mzazi huyo mwenzake bado anaendelea vyema licha ya hali ya kutatanisha inayomzunguka kwa sasa.

"Yuko shwari, hata niko naye," alisema.

Wakati huo huo, muigizaji huyo kijana alifichua kwamba mikakati ya hatua za kisheria dhidi ya aliyevujisha video hizo inaendelea.

Ingawa hakutoa maelezo mengi, Baha alifichua kwamba wanajiandaa kumshtaki mhusika kwa aibu aliyomletea mpenziwe. 

"Mipango inaendelea, tutachukua hatua za kisheria," alisema.

Hapo awali, Bi Georgina alikuwa amedai kwamba mpenzi wake wa zamani ndiye aliyehusika katika uvujishaji wa video hizo chafu.

Wakati akimjibu mwanablogu wa hapa nchini, alidokeza kuwa mpenzi wake huyo wa zamani  hakufurahishwa na uhusiano wake na Tyler.

"Ilitokea nikiwa na miaka 17 na mtu niliyempenda," alisema Georgina.

Aliongeza; "Alianza kunitisha mara tu baada ya kufichua uhusiano wangu na Tyler mwaka wa 2020."

Huku akimjibu mwanablogu, mwanamume huyo hata hivyo alidai kuwa shutuma hizo ‘hazina msingi wowote' na kuongeza kuwa, “Isipokuwa kama ana uthibitisho wowote kwamba nilivujisha picha za uchi."

Aliendelea kueleza kwamba walikuwa marafiki wa kufaidiana kwa muda mrefu.