Ex wa Mulamwah, Carrol Sonnie afurahia wakati mzuri na mpenzi wake (+video)

Muigizaji huyo alimficha sana mpenzi wake na alionyesha tu sehemu ya miguu yake.

Muhtasari

•Mzazi mwenza huyo wa Mulamwah alipakia video yake akiingia katika hoteli ya kifahari ambako alifurahia mlo mzuri.

•Mama wa binti mmoja pia alionyesha kidogo miguu ya mwanamume ambaye alikuwa ameenda kufurahia wakati na mlo naye.

Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Siku ya Jumatano jioni, muigizaji Caroline Muthoni almaarufu Carrol Sonnie alishiriki habari za kusisimua na mashabiki wake.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mzazi mwenza huyo wa mchekeshaji Mulamwah alipakia video iliyomuonyesha akiingia katika hoteli ya kifahari ambako alifurahia mlo mzuri.

Kwenye maelezo alifichua kuwa alikuwa ameenda nje kufurahia chakula cha jioni na mpenzi wake wa sasa.

"Nje kwa chakula cha jioni na mtoaji wangu wa ubavu," Carrol Sonnie alisema.

Kibiblia, wakati mwanamke anaposema mtoaji ubavu anamaanisha mpenzi wa kiume kwani inaaminika kuwa mwanamke aliumbwa kutoka kwa ubavu wa mwanaume.

Katika video hiyo, mama wa binti mmoja pia alionyesha kidogo miguu ya mwanamume ambaye alikuwa ameenda kufurahia wakati na mlo naye.

Mapema mwezi uliopita, Sonnie alidokeza alikuwa anateseka sana chini ya hali ya hewa ya baridi ilikuwa ikishuhudiwa kote nchini.

Katika taarifa kwenye threads, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kuwa hali ya hewa baridi ilimpa mawazo ya kumuita mpenzi wake wa zamani.

“Hii weather itafanya ni call ex.. excuses,” aliandika.

Hata hivyo hakutaja ni yupi kati ya wapenzi wake wa zamani ambaye alijaribiwa kumtafuta ili kusaidiana naye kukabiliana na baridi.

Kwa sasa, muigizaji huyo amekuwa akiweka mahusiano yake siri huku mzazi mwenzake, David Oyando almaarufu Mulamwah akidaiwa kuchumbiana na rafiki yake Ruth K.

Carrol Sonnie aliachana na mchekeshaji huyo mwaka wa 2021, kipindi kifupi tu baada ya wawili hao kubarikiwa na mtoto pamoja. Tangu wakati huo wamekuwa wakionyesha uhusiano wao mbaya hadharani mara kadhaa.

Wakati akithibitisha kutengana kwao mwezi Desemba mwaka 2021, Sonnie alisema walifanya makubaliano ya pamoja huku akimshukuru baba ya binti wake kwa kipindi cha miaka minne ambacho walikuwa pamoja.

"Hii ni kuweka wazi kuwa mimi na Mulamwah hatuko pamoja tena. Sote tumekubaliana na kuamua kuachana kwa sababu zinazojulikana kwetu. Asante sana kwa upendo na usaidizi mliotupa kwa miaka hiyo 4, mimi binafsi sichukulii kawaida.

Kwa mulamwah, Asante sana kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya maisha yako kwa miaka hiyo.  Nashukuru sana na nitahifadhi kumbukumbu milele. Katika hatua yako inayofuata maishani, sikutakii kingine ila bora.Endelea kushinda na Mungu akubarikikatika  kila hatua ya maisha yako," Muthoni aliandika.

Wapenzi hao  wa zamani walikaribisha mtoto wao wa kwanza wa kike, Keilah Oyando mnamo Septemba 20 mwaka wa 2021.