Maria Mtakatifu aonekana mbele ya waumini wakati wa ibada Kasarani (video)

Baadhi ya waumini walionekana wakirekodi tukio hilo huku wengine wakiinua mikono kupiga sala na kumsifu Mungu.

Muhtasari

โ€ขMaria Mtakatifu anadaiwa kutokea mbele ya waumini wa kanisa moja la Katokiliki katika eneo ya Kasarani, Nairobi.

โ€ขViongozi wa kanisa na waumini waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya ibada hiyo wanasikika wakipiga kelele na kusifu wakati picha hiyo ikioonyeshwa.

Image: HISANI

Mamake Yesu, Maria Mtakatifu anadaiwa kutokea mbele ya waumini wa kanisa moja la Katokiliki katika eneo ya Kasarani, Nairobi.

Video iliyofikia Radio Jambo inayodaiwa kuwa ya tukio hilo inaonyesha sura ya mwanamke ikiwa imemulikwa kwenye ukuta wa mbele ya Kanisa la Parokia ya St Clare. Viongozi wa kanisa na waumini waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya ibada hiyo wanasikika wakipiga kelele na kusifu wakati picha hiyo ikioonyeshwa.

Baadhi ya waumini walionekana wakirekodi tukio hilo huku wengine wakiinua mikono na kusema sala na kumsifu Mungu.

Tazama video hapa:-

Haijabainika kama kweli tukio hilo lilitokea au ilikuwa ni ukarabati wa teknolojia lakini Wakenya wameendelea kwa maoni mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, wengi wao wakionekana kulitupilia mbali.

Soma maoni ya baadhi ya wanamitandao Wakenya;

nimrodnick: ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚na unaniambia cocaine ndio dawa mbaya zaidi

christinewawira: Ikiwa mababu zetu wangeweza kuona kile ambacho tumekuwa sasa ๐Ÿ˜‚

brasho: Tunajua mwangaza wa projekta, watu sio wajinga buana

backyard_thriftplug: Sitaki kucomment vibaya nikose kuenda heaven ju ya comment tu๐Ÿ˜‚

misskithinji Mwenye aliambia watu Bikira Maria anakaa hivo ni nani?

boazinhoke utANASWAA EEEEEH๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚, the pastors wameshangaa kutushinda sisi wenye tuko nyumbani

ericnjiru: Patia Mary simu

me.see Hata nimevaa miwani na bado hakuna kitu naona