Mwanamitindo Miriam Odemba aweka wazi uhusiano wake na Ibraah

Odemba aliweka wazi kuwa uhusiano wake na Ibraah ni wa kirafiki tu.

Muhtasari

•Msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 hata hivyo alikiri upendo wake kwa Ibraah na hata kudokeza colabo yake naye.

•Takriban miezi mitatu iliyopita mwanamitindo huyo alikuwa amedai kuwa kwenye mahusiano na Ibraah.

Ibraah na Miriam Odemba
Ibraah na Miriam Odemba
Image: INSTAGRAM// IBRAAH

Mwanamitindo wa Bongo Miriam Odemba amezizima tetesi kuwa yupo kwenye mahusiano na msanii Ibraah wa Konde Gang.

Katika mahojiano na Carrymastory, Odemba aliweka wazi kuwa uhusiano wake na Ibraah ni wa kirafiki tu.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 hata hivyo alikiri upendo wake kwa Ibraah na hata kudokeza colabo yake naye.

"Jamani, Ibraah ni rafiki yangu. Ibraah nampenda sana, naweza nikatoa colabo na Ibraah. Msubirieni tu," Odemba alisema.

Takriban miezi mitatu iliyopita hata hivyo mwanamitindo huyo alikuwa amedai kuwa kwenye mahusiano na Ibraah.

Katika chapisho la Instagram, Odemba alisema kuwa Ibraah ndiye mume wa chaguo lake na kukiri kuridhika na mahaba yake.

"Nimemkolea Ibraah kwa sababu mtoto laini, mtoto safi, mwanaume asiye na maskendo na ndiye mume wangu mupige mniue. Huku chuma, huku sumaku niwaibie siri kabisa kwa hili Miriam Odemba siambiliki kabisa kwisha yenu habari," Alisema.

Alidokeza kuwa alivutiwa sana na sura ya Ibraah, mchezo wake wa kitandani na maisha yake rahisi yasiyozingirwa na drama nyingi.

"Hana maskendo ndioa maana napenda kukufa huyu mwanaume. Hilo swala la kuhangaika na watu wazima wenzangu kama wengine wanavyosema kwa sasa kwangu lipo likizo na inatakiwa mjue kwamba ukubwa jalala mtu mzima ni kutafutiana lawama za kutoridhishana mahabani. Sasa  ya nini yote hayo mimi sitaki lawama!" Odemba alisema.

Mwanamitindo huyo alikumbana na ukosoaji mkubwa mitandaoni baada ya kukiri mapenzi yake kwa Ibraah hasa kutokana na utofauti mkubwa wa kiumri. Wawili hao wameacha na takriban miaka 17.