"Nakumiss!" Kajala ashindwa kuvumilia upweke nyumbani baada ya Harmonize kusafiri

Muhtasari

•Kwa sasa Harmonize yupo ziara ya kimuziki jijini Goma, Congo na kwa kweli Kajala ameshindwa kuvumilia upweke nyumbani.

•Harmonize alifichua kwamba huwa raha kila anapopata fursa ya kushinda na mpenzi huyo wake nyumbani

Harmonize na Frida Kajala
Harmonize na Frida Kajala
Image: HISANI

Ni wazi kuwa penzi la Harmonize na Kajala limeendelea kutaradadi kila uchao baada ya wawili hao kurudiana wiki kadhaa zilizopita.

Kwa takriban mwaka mzima kulikuwa na uhusiano mbaya kati ya wasanii hao wawili kufuatia kutengana kwao Aprili mwaka jana. 

Hali hiyo hata hivyo ilibadilika wiki kadhaa zilizopita baada ya Kajala kukubali ombi la msamaha la Harmonize.

Kwa sasa bosi huyo wa Kondegang yupo katika ziara ya kimuziki jijini Goma, Congo na kwa kweli Kajala ameshindwa kuvumilia upweke nyumbani. 

Muigizaji huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha mahaba yake kwa Harmonize na kumueleza jinsi anayompeza.

"I miss you @harmonize_tz💉😣❤," Kajala alisema kwenye Instastori zake.

Ujumbe huo ulijiri masaa machache tu baada ya Harmonize kutengeneza video kwa ajili ya mpenzi huyo wake.

Katika video hiyo Harmonize alionyesha upendo mkubwa ambao anapokea Kongo na kusema kuwa yuko pale ili kumfanya Kajala ajivunie.

"Nataka ujue kuwa niko hapa na nakupeza sana. Najua uko mbali lakini sina la kufanya kwa sababu najua unajiandaa kwa siku yetu kubwa. Najuvunia wewe na niko hapa kukufanya ujivunie," Alisema.

Mwanamuziki huyo pia alitumia video hiyo kumshukuru mpenzi huyo wake kwa kumpa motisha ya kuchapa kazi yake ya muziki

"Niko hapa kukufanya ujivunie. Huu ni mwanzo tu wa kuhesabu baraka," Alisema.

Kwenye Instastori zake, Harmonize alifichua kwamba huwa raha kila anapopata fursa ya kushinda na mpenzi huyo wake nyumbani.

Ni wazi kuwa wawili hao tayari wameanza kuishi pamoja tena. Kajala sasa sio tu mpenzi wa Harmonize bali pia ndiye meneja wake.