Nimechumbiana na wanaume wa kila aina, nimetumiwa na nikaachwa- Diana Marua afunguka

Diana alisema anatamani mamake na mama ya Bahati wangekuwa hai ili kuungana nao kusherehekea mapenzi yao.

Muhtasari

•Diana alifunguka kuhusu matukio mabaya aliyopitia katika mahusiano yake ya awali kabla ya kukutana na mwanamuziki huyo.

•Diana alisema maisha yake yalibadilika alipokutana na Bahati kwani waliingiana vyema na kumfanya aachane na kila mtu mwingine.

Diana Marua
Diana Marua
Image: Instagram

Mwanavlogu maarufu Diana Marua amefunguka kuhusu safari yake ngumu hadi maisha mazuri ambayo anaishi kwa sasa.

Katika taarifa ndefu siku ya Jumanne jioni, mama huyo wa watoto watatu alijivunia hatua kubwa ambayo amepiga maishani katika muongo mmoja uliopita ikiwa ni pamoja na kuwa njiani kuolewa rasmi na mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati.

Diana alizungumzia changamoto nyingi ambazo alikumbana nazo alipokuwa anakua ikiwa ni pamoja na kutomaliza elimu kwa sababu ya ukosefu wa karo ya shule.

“Unaponitazama, unaona msichana wa Bahati lakini hujui imechukua nini hadi kufika hapa. Nimekumbana na nyakati ngumu sana nikikua, sikumaliza shule kwa sababu hakukuwa na pesa, kuwasihi wenye nyumba watupe siku chache zaidi ilikuwa utaratibu wa siku, tulikuwa na kitabu cha Mkopo, kwa duka hilo. tungelipa kila mwezi na hilo lilikuwa jambo la kawaida kwetu,” Diana alisimulia.

Aliongeza, "Niliacha shule na kazi yangu ya kwanza ilikuwa kuuza Line ya 'U' wakati mawasiliano ya muda mrefu yalipoanza nchini Kenya. Kisha baadaye nikawa ajenti wa Mpesa. Nilipiga hatua polepole kuelekea ulimwengu wa kibiashara na nikawa mpokeaji wa wageni aliyepuuzwa, lakini Mungu ni nani? Sikujua nitaishi katika jumba langu la kifahari, nitaendesha magari makubwa, kuwa mwajiri, nitawapa watoto wangu ulimwengu na kuishi maisha yaliyojaa Fadhili za Mungu, Baraka na Utele 😭😭😭.”

Kando na matatizo ya kifedha, mke huyo wa Bahati pia alifunguka kuhusu matukio mabaya aliyopitia katika mahusiano yake ya awali kabla ya kukutana na mwanamuziki huyo.

"Nimekuwa na sehemu yangu mwenyewe ya panda shuka za maisha. Nimechumbiana na wanaume wa kila aina, nimetumiwa na nimeachwa 😂 nimevunjwa moyo, nimepigwa lakini yote haya yalikuwa yakinitayarisha kwa mpango wa Mungu," alisema.

Diana alisema kuwa maisha yake yalibadilika alipokutana na mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili kwani waliingiana vyema na kumfanya aachane na kila mtu mwingine.

Pia alifichua kuwa uhusiano wao umefanikiwa kwa sababu ya kujitolea, uvumilivu, bidii, kusimama pamoja na kuomba msamaha mtu anapokosea.

“Kama ningepewa na ombi moja, ingekuwa kwa Mama zetu kushuhudia siku hii na kusherehekea nasi 😭 Lakini Mungu alikuwa na mipango mingine. Wanatutazama Mbinguni na najua tumewafanya wajivunie sana, " Diana alisema.

Mwanavlogu huyo aliendelea kumsifu mume wake na kumshukuru kwa kuitunza familia yao kwa upendo na heshima kubwa.