"Niruhusu nikusanye virago niondoke!" Akothee ajitenga na familia kufuatia ugomvi na mdogo wake

Mwimbaji huyo alifichua kuwa alimblock dadake baada ya kumtumia barua akieleza sababu ya kujitenga naye.

Muhtasari

•Akothee amedai kuwa ugomvi kati yake na mdogo wake umezidi kuwa mkubwa kwa kuwa mara nyingi familia yake ilikosa kuingilia kati.

•Alifichua kuwa wakati alipokuwa amelazwa hospitalini alimwandikia dadake barua akimueleza kwa nini lazima angejitenga naye.

Cebbie na dadake Akothee
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwimbaji mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amefunguka kuhusu ugomvi kati yake na dadake mdogo Cebbie Nyakokeyo.

Katika chapisho refu kwenye Facebook, amesema kuwa Cebbie sio dadake tu mbali alikuwa rafiki yake wa dhati hadi umaarufu ulipowatenganisha.

Amedai kuwa ugomvi kati yake na mdogo wake umezidi kuwa mkubwa kwa kuwa mara nyingi familia yake ilikosa kuingilia kati.

"Mambo yalitua kwenye meza yangu ambayo yalinivunja lakini hayakuniua🙏 ,tena hakuna mtu aliyenyoosha mkono , nilibaki kupambana peke yangu. Tena kama mkubwa wao mambo yalilazimishwa kwenye koo yangu. Nilikubali kuwa mkubwa hadi nilipopunguzwa kuwa mkeka wa mlangoni," alisema.

Mama huyo wa watoto watano amefichua kwamba alivunjika moyo zaidi wakati dadake mdogo alipodai kuwa anajifanya  katika kipindi ambacho alikuwa akipambana na msongo wa mawazo kwa takriban miezi sita.

"Niliporudi kwenye fahamu zangu, niliona ni vigumu kukubali ulikuwa mzaha, dada yangu hajawahi kunitembelea katika hospitali yoyote, si kwa njia mbaya lakini lazima alisafiri au kitu kama hicho, simlaumu,"

Alifichua kuwa wakati alipokuwa amelazwa hospitalini alimwandikia dadake barua akimueleza kwa nini lazima angejitenga naye.

Cebbie na dadake mkubwa Akothee
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Hata hivyo hakutuma barua hiyo hadi tarehe 31 Desemba mwaka jana kwa kuwa kila siku alitumai wangeweza kuzika uhasama wao. Alifichua kuwa alimblock dadake baada ya kupata ujasiri wa kutuma barua aliyokuwa amehifadhi kwa muda

"Nilisubiri dada yangu aje aseme (dada , unajua nini , samahani kwa maumivu yote niliyosababisha, tuzike yaliyopita na tujikusanye🙏) Hapana, familia iliendelea kusisitiza niwe wa kwanza kuenda kwake. Niliumia na kuumia, kwani sio mimi niliyesababisha tofauti, sio ile ninayoijua," alisema.

"Kweli, najivunia sana dada yangu, kutoka chini ya moyo wangu. Ninamtakia maisha bora zaidi, maisha yake ya baadaye yawe safi kama nyota. Nimemsamehe hadharani dada yangu, yuko na bado atabaki kuwa DAMU yangu."

Licha ya kukiri kuwa amemsamehe dada yake, aliweka wazi kuwa uhusiano kati yao hutawahi kuwa sawa tena. Pia alidokeza kwamba hatakuwa akihudhuria hafla za dadake na vilevile watu wasitarajie kumuona dadake katika hafla yake.

Aidha alitoa ombi kwa mashabiki, vyombo vya habari na wanablogu kujitenga na masuala ya familia yao na kuwaacha wayashughulikie wenyewe.

"Iwapo ujumbe huu pia umeharibu uhusiano kati yangu na wanafamilia wengine wasio na hatia tuliowaweka mengi yetu, nitakubali maamuzi yao na matokeo ya jinsi hii itaishia. Ilinibidi kufanya hivi ili niwe huru. WANAFAMILIA WAMEWAHI KUUWANA KWA KUWEKA MENGI NDANI. YAACHIENI NA MUWE HURU," alisema.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alitamatisha chapisho lake kwa ujumbe uliodokeza kuwa amejitenga na familia yake.

"Niligundua kuwa mimi ndiye mwenye sumu, niruhusu nikusanye virago na niondoke,"