"Ondokea shida, sio lazima upigane!" Samidoh amsihi mwanawe asifuate nyayo zake

Mwimbaji huyo alimshauri mwanawe kutorudia makosa ambayo yeye alifanya.

Muhtasari

•Siku ya Jumanne, Samidoh alionyesha barua nzuri aliyoandikiwa na mwanawe akikiri upendo wake mkubwa kwake.

•Desemba mwaka jana, mwimbaji huyo alijipata katika mzozo uliohusisha mke wake Edday na mzazi mwenzake Karen Nyamu.

Image: INSTAGRAM// SAMIDOH

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amempa mwanawe mkubwa ushauri maalum wa maisha.

Siku ya Jumanne, Samidoh alionyesha barua nzuri aliyoandikiwa na mwanawe akikiri upendo wake mkubwa kwake.

"Nakupenda baba,," ulisomeka mwanzo wa barua hiyo ikifuatiwa na maneno mengine machache yaliyofichwa.

Juu ya barua hiyo iliyoandikwa kwa mkono, mwimbaji huyo maarufu  aliandika, "Mvulana mkubwa na baba yake,"

Samidoh aliambatanisha ujumbe huo na sehemu fupi ya wimbo wa Country wa Kenny Rodgers,  'Coward of the County' ambapo anamsihi na kumshauri mwanawe kutorudia makosa ambayo mwenyewe alifanya.

"Niahidi mwanangu kutofanya yale niliyoyafanya. Ondokea shida ukiweza, haimaanishi kuwa wewe ni dhaifu ukigeuza shavu lingine. Natumai una umri wa kutosha kuelewa. Mwanangu, sio lazima upigane ili kuwa mwanaume," maneno ya wimbo huo ambayo aliweka kwenye posti yake yanasema.

Samidoh ni baba wa watoto watano wanaojulikana. Ana watoto watatu na mke wake Edday Nderitu, wasichana wawili na mvulana mmoja. Pia ana watoto wengine wawili na seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu.

Desemba mwaka jana, mwanamuziki huyo alikuwa  mzozo uliohusisha mke wake Edday na mzazi mwenzake Karen Nyamu. Mzozo huo ulitimbuka jijini Dubai ambako Samidoh aliratibiwa kutumbuiza.

Kizaazaa kilianza pale Karen alirushiana cheche za maneno makali naEdday baada ya kuenda mahali ambapo mwimbaji huyo alikuwa ameketi na mkewe na kumkalia kwenye mapaja kwa nguvu.

Bi Edday ambaye alionekana kukasirika hakuweza kustahimili dharau hiyo na akaamua kuchukua hatua.

Baadaye, Karen alitangaza kukatiza uhusiano na baba huyo wa watoto wake wawili wa mwisho kufuatia yaliyotokea.

"Wanawake wakubwa na wajasiri watathibitisha kwamba mara nyingi kiungo chetu dhaifu ni wanaume tunaojihusisha nao. Ninaacha mtindo huo," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram mwezi jana.

Aliongeza "Nimefanya uamuzi wa kusitisha uhusiano wangu na baba wa watoto wangu na sasa ni mpenzi wa zamani."

Alibainisha kuwa hakuwa na majuto yoyote kufuatia  kile kilichotokea Dubai, na kuahidi kuwa tukio hilo lilikuwa la mwisho.

"Sitamani ningefanya mambo kwa njia tofauti," Nyamu alisema. "Najua nilipaswa kumpigia simu na kumaliza kimya kimya, lakini niliamua kuweka hadharani kama jinsi tu drama mambo tatanishi yamekuwa," aliongeza.