Shinikizo lazidi kuongezeka kwa Diamond kumuoa zuchu

Babu Tale amewataka wawili hao kufunga pingu za maisha Desemba .

Muhtasari

•Diamond na Zuchu wamekuwa na uhusiano wa karibu mno kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja ambao umepita.

•Tale alithibitisha kuwa yeye kama meneja alitoa idhini ya tamasha hiyoambayo itafanyika katika Ramada Resort kuendelea.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Staa wa Bongo Diamond Platnumz amezidi kupata shinikizo kubwa la kufunga pingu za maisha na anayeaminika kuwa mpenzi wake wa sasa, Zuchu.

Diamond na Zuchu wamekuwa na uhusiano wa karibu mno kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja ambao umepita na kumekuwa na tetesi nyingi kuwa wasanii hao wawili wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Meneja wa Diamond, Babu Tale sasa amewataka wawili hao kufunga pingu za maisha mnamo siku ya kufunga mwaka huu, Disemba 31,  ambayo pia ndiyo siku ya  kuadhimisha kuzaliwa kwake. Tale amembainishia Diamond kuwa zawadi pekee anayotamani kutoka kwake mnamo siku hiyo ni harusi yake.

"Ombilangu kwa ndugu wasanii Diamond Platnumz na Zuchu hii tarehe ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu, najua kijana wangu Diamond vizawadi vya magari mara nyumba ni sehemu ya kawaida sana kwako ila mimi zawadi pekee utakayo nipa na itakayo ni furahisha siku hii kwanza upige ndoa hata ya watu wanne na mashahidi kadhaa inatosha.

Pili kwenye shoo mkaniimbie kwa pamoja nyimbo yangu pendwa wakati huo mkiwa bibi na bwana harusi kisha tunafunga na kufungua mwaka kwa sura mpya," Tale aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na bango la tamasha ya Diamond na Zuchu iliyoratibiwa kufanyika mnamo usiku wa mkesha wa mwaka mpya.

Tale alithibitisha kuwa yeye kama meneja alitoa idhini ya tamasha hiyoambayo itafanyika katika Ramada Resort kuendelea.

"Nilipo pigiwa kuhusu shoo ya tarehe 31/12 tena inafanyika Tanzania nilikua wakwanza kuishawishi ofisi iseme ndio,

Hii sio mara ya kwanza kwa Babu Tale kumshinikiza Diamond kufunga pingu za maisha na Zuchu. Mwezi Oktoba, wakati akitoa maoni chini ya video ya Diamond akionyesha mkufu wa thamani aliozawadiwa na Zuchu, Babu Tale alimuomba msanii huyo wake kufanya mipango ya harusi na malkia huyo wa Zanzibar.

"Fanya basi uoe unanichelewesha ujue," aliandika Babu Tale.

Diamond hata hivyo hakujibu ujumbe ule na badala yake aliifuta video hiyo ambayo ilikuwa imealika maoni mengi kwenye ukurasa wake.