“Sina mimba ingine!” Mulamwah awaonya vikali wanadada wanaomlilia awatunge mimba

Mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah amedai kuwa wanawake wengi wamekuwa wakimtumia jumbe wakiomba kumzalia.

Muhtasari

•Baba huyo wa watoto wawili aliwapa onyo wanawake wanaotaka awatunge mimba akibainisha kwamba hana ‘mimba’ ingine.

•Aliwaomba wanadada wanaompenda kudumisha upendo wao kwake kuwa wa kikazi na wasitarajie kupata mimba kutoka kwake.

Mulamwah na mpenzi wake Ruth K
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mchekeshaji mashuhuri wa Kenya David Oyando almaarufu Mulamwah amesema kwa utani kuwa wanawake wengi wamekuwa wakimtumia jumbe wakiomba kumzalia.

Katika chapisho kwenye Instagram, baba huyo wa watoto wawili hata hivyo aliwapa onyo wanawake wanaotaka awatunge mimba akibainisha kwamba hana ‘mimba’ ingine.

“Kijana cha kitale, full time hustler,” Mulamwah aliandika chini ya picha yake ambayo alichapisha siku ya Jumatano.

Aliendelea kudai jinsi ambavyo hapendi kuchapisha picha zake akijigamba kuwa wadada wengi huwa wanamfuata kwenye DM ili kumsihi awapachike mimba.

“BTW huwa sipendi kujipost sana kwa sababu huwa nasumbuliwa sana na madem eti anataka mimba, kindly ladies, sina mimba ingine,” alisema.

Baba wa watoto wawili aliwaomba wanadada wanaompenda kudumisha upendo wao kwake kuwa wa kikazi na wasitarajie kupata mimba kutoka kwake.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya mchekeshaji huyo kumkaribisha mtoto wake wa pili, Oyando Jr almaarufu Kalamwah.

Mulamwah na mpenzi wake Ruth K walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Februari 10 kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Wakati akitangaza habari hiyo njema, Mulamwah alieleza dhamira yake kubwa katika kujenga kumbukumbu na mwanawe.

“MUNGU NI MKUU , hatimaye kijana wetu yuko hapa , mrithi yuko hapa , MFALME yuko hapa - @oyando_jnr aka kalamwah, karibu duniani mwanangu, ni hisia nzuri zaidi ulimwenguni hatimaye kukuona na kukushikilia. siwezi kusubiri sisi kukua na kufanya kumbukumbu pamoja, "alisema.

Pia alimtambua mzazi mwenzake Ruth K, na kumshukuru kwa kumpa mtoto wake wa pili na kuwa naye kila wakati.

"Asante sana @atruthk kwa zawadi hii nzuri na ya kushangaza, asante kwa kuwa karibu nami kila wakati," alisema.

Aliongeza, “Ninahisi mzima tena, nahisi kurejeshwa, nina furaha , familia sasa zina furaha dunia nzima ina furaha , ♥️♥️ . Nakutakia maisha marefu na yenye afya tele kijana wangu na kila la kheri ulimwenguni. baraka tele. Karibu KALAMWAH !! maisha marefu oyando.”