"Hadi kifo kitenganishe" Omanga asifu ndoa huku akikabiliwa na madai ya video chafu

CAS Millicent Omanga alidokeza kwamba kudumisha ndoa kunahitaji hekima nyingi.

Muhtasari

•Millicent Omanga amesifu ndoa kwa njia isiyo ya moja kwa moja huku akikabiliwa na madai ya kashfa ya video chafu.

•Waziri Msaidizi huyo alionyesha pete yake kidoleni huku akiimba kuhusu ndoa.

CAS Millicent Omanga
Image: Facebook

Waziri Msaidizi katika wizara ya Masuala ya Ndani, Millicent Omanga amesifu ndoa kwa njia isiyo ya moja kwa moja huku akikabiliwa na madai ya kashfa ya video chafu.

Siku ya Jumatatu, Omanga alitumia wimbo wa The Saint Ministers 'Ndoa' kubainisha kuwa ndoa ni mpango takatifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kupitia wimbo huo, seneta huyo wa zamani alidokeza kwamba kudumisha ndoa kunahitaji hekima nyingi.

"Ndoa ni mpango takatifu tangu mwanzo,

Ujumbe njema, utokao kwa baba,

Yahatijika hekima kuitunza,

Hadi kifo kiwatenganishe," Aliimba pamoja na The Saint Ministers katika video aliyoichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii

CAS huyo aliweka uso wa furaha huku akiimba maneno ya wimbo huo. Pia alionyesha pete yake huku akiimba kuhusu ndoa.

Mapema wiki jana, video ya mwanamke aliye uchi iliyorekodiwa wakati usiojulikana ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya Wakenya wakidai mhusika ni CAS Omanga. Hata hivyo, hakuna kilichothibishwa kufikia sasa.

Jumamosi wiki iliyopita, seneta huyo wa zamani alionekana kuvunja kimya kuhusu suala hilo kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Alionekana kutuma ujumbe wa tahadhari kwa mtu aliyehusika katika video hiyo inayovuma.

"Karma anasema, unapoharibu maisha ya mtu kwa uongo, ichukue kama mkopo. Itarudi kwako na riba, "alisema kwa kutumia nukuu.

Omanga aliendelea kuwahutubia walio nyuma ya kitendo hicho cha kutia aibu kwa kutumia wimbo wa injili ambapo alionekana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa naye licha ya majaribio yaliyomkumba hivi majuzi.

Katika akaunti yake ya  mtandao wa TikTok, alichapisha video yake akicheza na wimbo wa Yona Chilolo 'Nakutegemea Baba.'

"Wamejipanga kila kona wanataka kunidhuru,

Wanamatamani tukionana niwe nakosa uhuru.

Ata nifanye jambo njema sina wa kunishukuru,

Wangemiliki amani yangu ningelipiea ushuru.

Asante Mungu umenipenda ukanipa Uhuru,

Furaha yangu ninaipenda sitishwi na machungu

Ninakushuru Mungu wewe hauna mafungu,

Ukitaka kubariki hauzuiwi na mtu," aliimba na kucheza.

Katika takriban wiki moja iliyopita, Wakenya wamejaajaa kwenye mitandao ya kijamii wakitoa maoni kuhusiana na suala hilo, baadhi wakiwa na maoni hasi huku wengine wakimpa pole na kumtia moyo seneta huyo wa zamani.