'Wamejipanga wanataka kunidhuru!" Omanga amkimbilia Mungu baada ya video chafu kusambazwa

Omanga alituma ujumbe wa onyo kwa mtu aliyehusika katika video hiyo inayovuma.

Muhtasari

•Siku ya Jumamosi, seneta huyo wa zamani alionekana kuvunja kimya kuhusu suala hilo kwa njia isiyo ya moja kwa moja. 

•Omanga alionekana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa naye licha ya majaribio yaliyomkumba hivi majuzi.

CAS MIllicent Omanga
Image: FACEBOOK

Waziri Msaidizi katika Wizara ya Masuala ya Ndani Millicent Omanga hatimaye ameibuka tena baada ya siku kadhaa za kuvuma kwenye mitandao ya kijamii.

Mapema wiki hii, video ya mwanamke aliye uchi iliyorekodiwa wakati usiojulikana ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya Wakenya wakidai mhusika ni CAS Omanga. Hata hivyo, hakuna kilichothibishwa ama kukanwa kufikia sasa.

Siku ya Jumamosi asubuhi, seneta huyo wa zamani alionekana kuvunja kimya kuhusu suala hilo kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Alionekana kutuma ujumbe wa tahadhari kwa mtu aliyehusika katika video hiyo inayovuma.

"Karma anasema, unapoharibu maisha ya mtu kwa uongo, ichukue kama mkopo. Itarudi kwako na riba, "alisema kwa kutumia nukuu.

Omanga aliendelea kuwahutubia walio nyuma ya kitendo hicho cha kutia aibu kwa kutumia wimbo wa injili ambapo alionekana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa naye licha ya majaribio yaliyomkumba hivi majuzi.

Katika akaunti yake ya  mtandao wa TikTok, alichapisha video yake akicheza na wimbo wa Yona Chilolo 'Nakutegemea Baba.'

"Wamejipanga kila kona wanataka kunidhuru,

Wanamatamani tukionana niwe nakosa uhuru.

Ata nifanye jambo njema sina wa kunishukuru,

Wangemiliki amani yangu ningelipiea ushuru.

Asante Mungu umenipenda ukanipa Uhuru,

Furaha yangu ninaipenda sitishwi na machungu

Ninakushuru Mungu wewe hauna mafungu,

Ukitaka kubariki hauzuiwi na mtu," aliimba na kucheza.

Siku ya Jumanne asubuhi, Waziri huyo msaidizi katika wizara ya usalama wa ndani alivunja kimya kwa mara ya kwanza baada ya kile kilichodaiwa kuwa video yake ya utupu kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, Omanga alinukuu Bilbia yenye kifungo cha kujiliwaza ambapo Mungu anawaambia waja wake kwamba amewapa nguvu na hakuna kitakachowaumiza.

“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru." Luka 10:19. Siku njema wadau,” aliandika.

Katika siku chache zilizopita, Wakenya wamejaajaa kwenye mitandao ya kijamii wakitoa maoni kuhusiana na suala hilo, baadhi wakiwa na maoni hasi huku wengine wakimpa pole na kumtia moyo seneta huyo wa zamani.

Alhamisi,Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo alitoa onyo kali kwa wanaosambaza picha chafu za wanawake mashuhuri.

Akizungumza wakati wa kikao cha bunge, Bi Odhiambo aliwataka DCI kujitahidi kuwakamata wanaojihusisha na vitendo kama hivyo.

Odhiambo ambaye alisema amekerwa sana na kisa cha hivi majuzi ambacho kilimhusisha CAS Millicent Omanga alitaka sheria ifanyiwe marekebisho ambapo adhabu kali zitatolewa kwa watu wanaosambaza picha chafu za wanawake.

"Siungi mkono hukumu ya kifo, lakini natamani ningefanya hivyo. Kama ningekuwa naunga mkono hukumu ya kifo, ningeunga mkono hukumu ya kifo kwa watu kama hao," alisema."

"Lakini kwa sababu siungi mkono hukumu ya kifo, nadhani tunahitaji kuongeza hukumu kuwa  kifungo cha maisha kwa watu kama hao,"

Mbunge huyo wa ODM alitaka viongozi wengine Bungeni kuunga mkono muswada wa adhabu kali kwa washukiwa wa vitendo hivyo.

Alisema kkuwa watu wanapaswa kuzingatia madhara ya vitendo vyao kabla ya kuchukua hatua ya kusambaza picha kama hizo.

"Angalau kama hujali mhusika, wahurumie watoto wake," alisema.