"Nimepewa amri na nguvu zote, hakuna kitakachonidhuru!" - Millicent Omanga avunja kimya!

Waziri msaidizi huyo amenukuu kifungu hiki saa chache baada ya video inayodhaniwa kuwa yake ya utupu ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii.

Muhtasari

• Kifungu cha 31 cha Katiba ya Kenya kinataja kuwa hatia mtu kusambaza picha chafu za mtu bila idhini.

• Ni kosa ambalo linaweza kusababishia faini isiyozidi laki mbili au kufungwa miaka miwili jela au yote mawili.

Millicent Oamnga kuhusu suala la kitambi kwa wanawake
Millicent Oamnga kuhusu suala la kitambi kwa wanawake
Image: Facebook

Waziri msaidizi mteule katika wizara ya usalama wa ndani Millicent Omanga amevunja kimya chake baada ya kile kinachodhaniwa kuwa ni video yake ya utupu kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Omanga alinukuu Bilbia yenye kifungo cha kujiliwaza ambapo Mungu anawaambia waja wake kuwa amewapa nguvu na hakuna kitakachowaumiza.

“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru." Luka 10:19. Siku njema wadau,” Omanga aliandika.

Hata hivyo, haijabainika iwapo ni kweli video hiyo inayoenezwa ikimuonesha akiwa nusu uchi ni yeye ama ni wat utu wenye nia mbaya waliamua kufanya uhariri wa sura yake kwenye picha ya mtu tofauti.

Kwa kawaida picha za utupu zinapovujishwa kwenye mitandao ya kijamii huwaunganisha Wakenya Zaidi ya kitu chochote kile.

Na tangu usiku wa Jumatatu, Omanga amekuwa gumzo la mitandao yote ya kijamii kisa tu video hiyo ambayo baadhi wanadai ni yeye na sehemu ya mashabiki wake wakipinga vikali kuwa kuna mtu aliyekuwa na njama fiche ya kumharibia jina aliyekuwa mgombea wa uwakilishi wa kike Nairobi, Millicent Omanga.

Baadhi ya mashabiki wake kwenye Facebook walifurika chini ya dakika chache za kupakia kifungu hicho cha Biblia wakimtaka kuwa imara na kutotishiwa na mtu yeyote.

“Amen, napenda himizo ndani yako, endelea kusimama imara,” mmoja alimwambia.

“Kiongozi mzuri anawaunganisha wananchi, ahsante kwa kutuungansiha,” mmoja alimtania akirejelea video ile.

Hata hivyo, Omanga hajaweka wazi kama video ile ni yake na wala hajadokeza hatua zozote za kisheria atakazozichukua iwapo kweli ni video yake ilivujishwa.

Nchini Kenya kisheria, ni hatia kwa mtu kuvujisha utupu wa mwenzake mitandaoni na ni sheria iliyopitishwa 2018 na rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Sheria chini ya kifungu cha 31 kwenye katiba ya Kenya ambacho kinaunda kosa kinaeleza;

‘Mtu anayehamisha, kuchapisha, au kusambaza, ikiwa ni pamoja na kufanya taswira ya dijiti ipatikane kwa ajili ya kusambazwa au kupakuliwa kupitia mtandao wa mawasiliano ya simu au kwa njia nyingine yoyote ya kuhamisha data kwa kompyuta, picha ya karibu au chafu ya mtu mwingine anatenda kosa na atawajibishwa kisheria, akitiwa hatiani kwa kulipa faini isiyozidi shilingi laki mbili au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.’