Mume apakia picha chafu kwenye akaunti ya mpenziwe na kubadilisha 'password' alipoachwa!

Baada ya kuachwa, kijana huyo aliamua kulipiza kisasi kwa kuiba akaunti ya mpenzi wake na kuchapisha picha na video zake akiwa uchi.

Muhtasari

• Kesi hiyo inadai kuwa Hunter, mpenzi wa zamani wa mwanamitindo huyo, alichapisha 'picha nyingi, na video chafu za Saravia.

• Saravia aliweza kuchukua udhibiti wa akaunti zake muda mfupi baadaye.

Mikayla Saravia na aliyekuwa mpenzi wake Nicholas Hunter.
Mikayla Saravia na aliyekuwa mpenzi wake Nicholas Hunter.
Image: Instagram

Mwanamitindo mmoja ameelekea mahakamani kumshtaki mpenzi wake wa kiume kwa kuiba akaunti yake ya mtandao wa kijamii kisha kupakia picha chafu kama njia moja ya kulipa kisasi kwa kuachwa.

Mikayla Saravia, 25, anadai kuwa Nicholas Hunter, 27, alibadilisha nywila kwenye akaunti yake na kuchapisha picha na video zake chafu baada ya kutengana mwezi Oktoba, kulingana na kesi ya kulipiza kisasi ya utupu iliyowasilishwa katika mahakama ya shirikisho wiki hii.

Katika kesi hiyo, mwanadada huyo anataka kulipwa shilingi bilioni 771 sawa na dola za Marekani bilioni 6.3 kwa kuchafuliwa picha na jina lake mitandaoni.

Saravia - ambaye ana mamilioni ya mashabiki kwenye tovuti nyingi za mitandao ya kijamii - ana akaunti mbili kwenye OnlyFans - moja ambayo ni ya bure na moja 'wazi' zaidi ambayo inampa mapato ya $30 kwa mwezi, jarida moja liliripoti.

Kesi hiyo inadai kuwa Hunter, mpenzi wa zamani wa mwanamitindo huyo, alichapisha 'picha nyingi, na video chafu za ngono' na video za Saravia, zikiwemo za kuuzwa, kuanzia Oktoba 2022 hadi Januari 2023.

Saravia aliweza kuchukua udhibiti wa akaunti zake muda mfupi baadaye.

Wakili wake Joseph DiRuzzo alikiri kuwa mteja wake alikuwa amechapisha maudhui ya utupu akiwa peke yake, lakini akadokeza kuwa yeye ndiye aliyekuwa na udhibiti wa machapisho hayo kipindi hicho.

"Kwa sababu tu uliidhinisha picha hapo awali, haimaanishi kuwa unampa mtu ruhusa ya kuchapisha maudhui ya ziada bila idhini yako," DiRuzzo aliandika kwenye malalamiko hayo kulingana na jarida hilo.