"Maisha yangu yako hatarini" Akothee ahofia maisha baada ya kushambuliwa, akimbilia polisi

Mwimbaji Akothee amezua wasiwasi kuhusu maisha yake akidai kuwa alishambuliwa Jumatano asubuhi.

Muhtasari

•Akothee alidai kuwa alishambuliwa na wahuni wasiotambuliwa alipokuwa katika afisi moja ya serikali ya kaunti ya Migori.

•Akothee alisema kuwa polisi walimsindikiza nje ya kaunti ya Migori baada ya kurekodi taarifa katika kituo cha polisi.

Akothee
Akothee
Image: HISANI

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amezua wasiwasi kuhusu maisha yake akidai kuwa alishambuliwa Jumatano asubuhi.

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alidai kwamba maisha yake yako hatarini akidokeza kuwa baadhi ya wanasiasa kutoka kaunti ya nyumbani kwao Migori ambao hawakutajwa majina wanamlenga.

Alidai kuwa alishambuliwa na wahuni wasiotambuliwa alipokuwa katika afisi moja ya serikali ya kaunti kisha akaenda katika kituo cha polisi na kupiga ripoti.

“Kwa hivyo, maisha yangu yako hatarini katika Kaunti ya Migori, sikuona haya yakija. 🙏 Sawa kama wanasiasa wa Migori wanataka kuniua msitumie wahuni kupitisha habari zenu nipigeni risasi tu,” Akothee alisema Jumatano alasiri.

Aliongeza, “Nimeona ufunuo wa Mungu asubuhi ya leo, nitawajuza baadaye. Uchunguzi bado unaendelea. Niko katika kituo cha polisi baadhi ya wahuni walinivamia asubuhi ya leo katika Ofisi ya Waziri wa Fedha ya Kaunti ya Migori. Walikusanyika mbele ya mlango wakitarajia nitoke kupitia mlango uleule. Nilitoka na mlango wa nyuma. Mara wakagundua nimetoka wakakimbia kunizuia getini. Walinzi wa kaunti walikuja wakacheka nao na kuondoka pale wakisema watanionyesha vumbi huko Migori 🤔."

Mama huyo wa watoto watano Alidai kuwa alishambuliwa na wahuni wasiotambuliwa alipokuwa katika afisi moja ya serikali ya kaunti

Aliambatanisha madai yake na video inayoonyesha gari la polisi likifuata gari lake alipokuwa akisindikizwa kutoka katika kaunti yake.

"Haitafaulu kuwaingiza shule Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza leo ambayo ilikuwa ya kutisha 🙏Inazidi kuwa fujo," alisema.