#MamaTetema yake Rayvanny yatetemesha chati za muziki mexico

Muhtasari

• Ngoma ya Rayvanny, #MamaTetema imerekodiwa kufanya vizuri kwenye chati tofauti za muziki nchini Mexico.

• Star huyo wa bongo alichapisha katika ukurasa wake wa Instagram kusherehekea hatua hiyo . Hii ilikuwa collabo aliyoifanya na msanii Maluma kutoka taifa la Colombia.

• Wasanii mbalimbali wa Tanzania wakiwemo Maua Sama na Billnass wamejitokeza kumpongeza Rayvanny kufuatia hatua hiyo.

Ngoma ya Rayvanny, #MamaTetema imerekodiwa kufanya vizuri kwenye chati tofauti za muziki nchini Mexico.

Star huyo wa bongo alichapisha katika ukurasa wake wa Instagram kusherehekea hatua hiyo. Hii ilikuwa collabo aliyoifanya na msanii Maluma kutoka taifa la Colombia.

Kulingana na Rayvanny, hizi ndizo takwimu za ngoma hiyo pale Mexico:

Mexico Airplay - #1

Mexico Espanyo- #5

Latin Rhythm airplay- #18

Latin Airplay-#41

Ikumbukwe kwamba 'Chui' aliwahi kufanya kolabo ya kibao #Tetema na boss wake, Diamond Platinumz ila ngoma hiyo haikufanya vizuri katika mataifa ya ughaibuni Kama hii aliyoshirikiana na msanii Maluma kutoka Colombia.

Wasanii mbalimbali wa Tanzania wakiwemo Maua Sama na Billnass wamejitokeza kumpongeza Rayvanny kufuatia hatua hiyo.

Tukio hili linajiri huku Rayvanny akikisiwa kuondoka WCB ambapo amejenga kipaji chake Cha kuimba.