'Wakunywe waongee vizuri sasa,'Fridah Kajala amwambia mwanawe baada ya kuwasili Tanzania

Muhtasari
  • Mama yake amekuwa akichapisha kila mara kwenye mitandao ya kijamii akidai kuchoshwa na kumkosa bintiye Vibaya
  • Hata alithibitisha kuwa hajawahi kuwa mbali na binti yake kwa muda huo
Muigizaji Fridah Kajala
Image: Fridah Kjala/INSTAGRAM

Paula na mama yake wametengana kwa muda mrefu . Hii ilikuwa baada ya Paula kwenda nje ya nchi kusomea udaktari katika Instabul Uturuki katika Chuo Kikuu cha Maltepe.

Mama yake amekuwa akichapisha kila mara kwenye mitandao ya kijamii akidai kuchoshwa na kumkosa bintiye Vibaya.

Hata alithibitisha kuwa hajawahi kuwa mbali na binti yake kwa muda huo.

Kupitia kwenye hadhithi za instagram muigizaji huyo alichapisha video akiwa kwenye uwanja wa ndege alipokuwa akimsubiri binti yake.

Punde  Paula walitua wote wawili walikumbatiana huku wakilia. Mama yake alikuwa akimsifu akimwambia kwamba amekua mkubwa na amekomaa.

Hata alimwambia aendelee kung'aa na kuvutia watu.

"Umekua mkubwa mwanangu sana na ukakomaa . Karibu Tanzania sasa nyumbani . Wakunywee Sasa Waongee Vizuri I got your back ," Fridah alimwambia mwanawe.

Siku ya JUmanne Frida alitumia uurasa wake wa insgram pia kuwaonya wakosoaji wake ambao wamekuwa wakimkejeli mwanawe kwa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msanii Rayvanny.

Fridah kwa hisia aliwaomba watu waache kumtuhumu binti yake kwani alisema mapenzi hayana mipaka.