Milly Chebby aomba mimba ya pili

Muhtasari

• Mkewe msanii Terrence Creative, Milly Chebby amedokeza kwamba anataka mtoto wa pili.

• Chebby anavyojulikana na wengi, Jumatano tarehe 26/01/2022 alichapisha kwenye Instagram picha yake ya awali huku akiambatanisha kauli iliyokuwa ikimsaili mumewe Kama yupo tayari kupokea mtoto wa pili.

• Wawili hawa pia wameanzisha biashara ya kukodi nyumba, wakiomba yeyote atakayetaka kuwekeza kwenye biashara hiyo kuwafikia kupitia mitandao ya kijamii.

Milly Chebby
Image: Milly Chebby/INSTAGRAM

Mkewe msanii Terrence Creative, Milly Chebby amedokeza kwamba anataka mtoto wa pili.

Chebby anavyojulikana na wengi, Jumatano tarehe 26/01/2022 alichapisha kwenye Instagram picha yake ya awali huku akiambatanisha kauli iliyokuwa ikimsihi mumewe Kama yupo tayari kupokea mtoto wa pili.

"#TBT exactly three years ago today sijui kama @Terrece Creative uko ready for round 2," alisema Chebby.

Image: INSTAGRAM// MILLY CHEBBY

Kauli hii inajiri siku chache tu baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo alitimu miaka 35. Siku hiyo alimuuliza mumewe kuwa angetaka ampe zawadi gani ambapo Terrence Creative alisema kwamba angependa wajaaliwe na mtoto wa pili, hii ikiwa ishara kwamba pengine Chebby amewazia swala hilo na sasa yupo tayari kubemba ujauzito kwa mara ya pili.

Wawili hawa pia wameanzisha biashara ya kukodi nyumba, wakiomba yeyote atakayetaka kuwekeza kwenye biashara hiyo kuwasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii.

Ni dhahiri kwamba wamejituma katika kazi zao na wanafanya kila wawezalo kupanga maisha yao ya halafu.