Mungai Eve na mpenziwe wanunua 'dinga' jipya.

Muhtasari

• Mzalishaji wa vipindi katika mtandao wa YouTube, Mungai Eve na mchumba wake hatimaye wamenunua gari jipya.

• Wapenzi hao ambaokatika siku za hivi karibuni wameonekana kuwa mabalozi wa kampuni mbalimbali wamekuwa kwenye sekta hii kwa takribani miaka miwili na hakika bidii yao inazidi kuwashajiisha vijana wengi kujituma katika maisha.

• Trevor ambaye ni mpenzi wake Mungai amechapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram kusherehekea hatua hiyo.

instagram KWA HISANI
instagram KWA HISANI
Image: mungai eve

Mzalishaji wa vipindi katika mtandao wa YouTube, Mungai Eve na mchumba wake hatimaye wamenunua gari jipya.

Trevor ambaye ni mpenzi wake Mungai amechapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram kusherehekea hatua hiyo na pia kumshukuru Evekwa kumuaminia katika kazi ambayo amefanya kuhakikisha kwamba jina lake linaingia katika orodha ya watu wenye ushawishi mkubwa hapa nchini Kenya katika mtandao wa YouTube.

"WELCOME HOME BABY️, ITS GOOD TO HAVE YOU JOIN US FINALLY.THANK YOU @Mungai_eve FOR ALWAYS BELIEVING IN ME," aisema Trevor.

Wapenzi hao ambaokatika siku za hivi karibuni wameonekana kuwa mabalozi wa kampuni mbalimbali wamekuwa kwenye sekta hii kwa takribani miaka miwili na hakika bidii yao inazidi kuwashajiisha vijana wengi kujituma katika maisha.

Awali katika moja ya video ambayo waliachia kwenye YouTube, Mungai Eve alisema kuwa gari hilo ni kama tuzo kwake Trevor kazi nzuri ambayo anaifanya. Kwa upande mwingine kumekuwa na presha kutoka kwa mashabiki kwa Trevor kufanya harusi ili kurasmisha mahusiano yao ila amesema anahitaji muda zaidi na pindi akiwa tayari kila kitu kitafanikishwa.