Davido amnunulia meneja wake gari lenye thamani ya $20.4k

Muhtasari

• Msanii wa Nigeria Davido amemnunulia meneja wake, Asa Asika  gari lenye thamani ya dola elfu ishirini.

• Gari hilo aina ya Toyota linagharimu takribani dola eflu ishirini [$20.4], ni ishara ya kumpongeza meneja huyu kwa kazi nzuri anayoifanya na kuhakikisha jina la msanii wake linazidi kuvuma katika kona zote za ulimwengu.

Msanii DAVIDO
Msanii DAVIDO
Image: INSTAGRAM// DAVIDO

Msanii wa Nigeria Davido amemnunulia meneja wake, Asa Asika  gari lenye thamani ya dola elfu ishirini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Asika amemshukuru bosi wake kwa kitendo hicho cha ukarimu na kuweka wazi furaha yake ya kuwa mmiliki wa gari jipya.

"I' m Now a Car Owner.. Thanks To My Oga @davido,” aliandika Asa Asika.

Gari hilo aina ya Toyota linagharimu takribani dola eflu ishirini [$20.4], ni ishara ya kumpongeza meneja huyu kwa kazi nzuri anayoifanya na kuhakikisha jina la msanii wake linazidi kuvuma katika kona zote za ulimwengu.

Àsa Asika ambaye alianza kazi ya kuwa meneja wa Davido mnamo mwaka wa 2008, ameonyesha mapenzi na ufahamu wake katika muziki kwa jinsi ambavyo ameonekana kushughulikia masuala yote ya kimuziki ya msanii wake.