Niliwahi kuwa na nyumba ya vyumba 5 lakini nilikuwa natumia chumba kimoja tu! - Huddah Monroe

Muhtasari

• Mwanasosholaiti Huddah Monroe amesema kwamba kuna wakati mmoja furaha yake ilikuwa ni kuwafurahisha watumizi wa mitandao kwa kumiliki vitu mbali mbali vyenye thamani ya juu.

Monroe amesema kwamba kuishi Maisha ya kawaida haina maana kwamba mtu amefilisika.

Huddah Monroe
Image: Facebook

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amesema kwamba kuna wakati mmoja furaha yake ilikuwa ni kuwafurahisha watumizi wa mitandao kwa kumiliki vitu mbali mbali vyenye thamani ya juu.

Huddah hivi majuzi alitangaza kupeana kama zawadi nyingi za nguo zake ambazo anasema hana maana nazo kwa sababu huwa anavaa mara moja tu.

Mwanamitindo huyo ameweka kwenye Instagram yake na kusema kwamba kwa wakati mmoja aliwahi miliki nyumba yenye vyumba vitano lakini cha kushangaza ni kwamba alikuwa anakitumia chumba kimoja tu huku vyumba vingine vikiwa vimejaa vitu ambavyo hakuwa anavitumia wala kuvihitaji katika Maisha yake.

Image: Instagram

Huddah amesema kwamba alikuwa na mazoea ya kumiliki vitu vingi hivyo ili kuwafurahisha mashabiki wake kwenye mitandao na sasa amesema ameacha hulka hizo kwani ni mambo yasiyo na maana kabisa katika maisha.

“Ninataka niwe mtu wa kubana matumizi. Kama ninaishi peke yangu, nyumba ya vyumba viwili inanitosha. Niliwahi ishi maisha ghali kwenye nyumba kubwa lakini sikupata faraja ya kibinafsi kutokana na maisha hayo,” aliandika Monroe

Image: Instagram

Akionekana kugusia madai yanayosambazwa kwenye mitandao kuhusu kutokuwa na gari kwa mwanamitindo mwenza kutoka nchi Jirani ya Tanzania, Wema Sepetu, Monroe amesema kwamba kuishi maisha ya kawaida haina maana kwamba mtu amefilisika.