Waah ya Diamond Platnumz, views milioni mia moja

Muhtasari

• Video ya ngoma yake Diamond Platinumz #Waah imetazamwa [views] na watu milioni moja katika mtandao wa YouTube huku audio yake ikitinga views milioni 3.3 mwaka mmoja tangu kibao hicho kidondoshwe.

• Ifahamike kwamba ngoma hiyo ilikuwa ni collabo kati ya Diamond Platinumz ambaye alipewa shavu na gwiji kutoka Congo Koffi Olomide , kuandaa kazi hiyo ambayo iliwateka mashabiki kwa asilimia kubwa mno.

Diamond Platnumz
Image: Hisani

Video ya ngoma yake Diamond Platinumz #Waah imetazamwa [views] na watu milioni moja katika mtandao wa YouTube huku audio yake ikitinga views milioni 3.3 mwaka mmoja tangu kibao hicho kidondoshwe.

Ifahamike kwamba ngoma hiyo ilikuwa ni collabo kati ya Diamond Platinumz ambaye alipewa shavu na gwiji kutoka Congo Koffi Olomide , kuandaa kazi hiyo ambayo iliwateka mashabiki kwa asilimia kubwa mno.

Hii ni moja kati ya ngoma zake Simba ambazo zimefanya vizuri zaidi tangu atie guu katika muziki wa bongo na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Sammisago
Sammisago
Image: Instagram KWA HISANI

Mashabiki sasa wanajiuliza iwapo waanii hawa wawili wataingia studioni kwa mara ya pili ili kuandaa ngoma nyingine, hili likiwa ni swala la muda kuona iwapo litatimia.

Diamond Platinumz anasubiriwa kuachia album yake ambayo meneja wake wamesema kwamba itatoka katika wakati mwafaka.