Zari Hassan aonekana na mwanamume mdogo kiumri

GK Choppa
Image: Instagram

Aliyekuwa mke wa staa wa muziki wa bongo fleva, Diamond Platnumz ameonekana akiwa kwenye kumbato na mwanaume anayedaiwa kuwa mdogo kiumri.

Katika picha zilizotembezwa mitandaoni, Zari anaonekana katika picha mbali mbali na mwanaume huyo ambaye wajasusi wa mitandaoni wamemtambua kwa jina GK Chopa ambaye ni Mganda anayesemekana kumpokelea Zari jijini Durban, Afrika Kusini alikoenda kwa ziara ya tafrija wikendi iliyopita.

Zari ambaye ni mama wa Watoto watano na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz alionekana katika mrundiko wa picha zilizopakiwa kwenye ukurasa wa Instagram wa mwanaume huyo, picha zikiashiria kabisa wawili hao wakiwa wanafurahia muda mwafaka wa maisha yao.

GK Choppa
Image: Instagram

Katika baadhi ya picha hizo, wawili hawa walionekana katika kumbato la kuashiria wawili waliopoteleana kwa muda mrefu kukutana.

 Baada ya picha hizo kuzua mijadala mikali kwenye mitandao, mfanyabiashara Zari amejitokeza wazi na kukana kwamba hakuna chochote kinachoendelea baina yao zaidi ya urafiki tu. Pia amewataka wambea kujishughulisha na mambo yao na kuacha kufuatilia maisha ya watu.

“Patia watu wa Afrika mashariki picha, na wataibuka na aya ndefu za maneno ambao wenyewe ndio wanajua. Kufuatilia mambo ya watu kutakuponza na hakuna atakayeshughulika na wewe!” Zari alisema.

Madai haya ya mfanyibiashara Zari yanakuja siku chache tu baada ya fununu kwamba mzazi mwenziwe Diamond anapanga kufanya harusi na msanii Zuchu mnamo Februari 14, na wengi walioingia kwenye mijadala mitandaoni kuhusu picha hizo za Zari wanahoji kwamba ni njia moja ya kujibu mipigo juu ya sakata la ndoa ya Diamond.