Raila, Musindi watoa wimbo wa kampeni

Muhtasari

• Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anatarajiwa kuzindua wimbo mpya alioshirikishwa na msanii Emmanuel Musindi kwa ajili ya kampen

• Februari 14 usiku, Raila aliweka kwenye mtandao wake wa Twitter na kusema kwamba wimbo wake mpya na msanii Musindi umepikwa na upo tayari kupakuliwa kwa wakenya kesho yake.

kinara wa ODM Raila Odinga
kinara wa ODM Raila Odinga
Image: Hisani

Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anatarajiwa kuzindua wimbo mpya alioshirikishwa na msanii Emmanuel Musindi kwa ajili ya kampeni za muungano huo kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9

Raila ambaye wengi wanamjua kama mwanasiasa mkongwe sasa amejiongezea taji lingine jipya la kuingia kwenye rekodi za wasanii wa ngoma humu nchini.

Katika wimbo huo ambao ameshirikishwa na Musindi, Raila walifanya remix ya ngoma ya awali ya msanii huyo almaarufu Leo ni Leo na video ya ngoma yenyewe inatarajiwa kushuka Februari 15 huku wengi wa wafuasi wa Raila wakiingojea kwa raghba ya mkanja kuona anavyoisakata.

Muongozaji wa muziki Maji Maji katika mahojiano na Mpasho alisema kwamba Raila akiwa studioni kwa ajili ya kurekodi remix hiyo alionekana mstaarabu na mwenye utulivu mkubwa

Wimbo huo wa Musindi umekuwa ni miongoni mwa ngoma pendwa sana na Raila haswa katika misafara yake ya kisiasa kote nchini tangia aanze rasmi kupiga kampeni

Video hiyo ambayo ilichukua muda wa siku moja kufanyika na mtayarishaji mashuhuri Nezzoh inatarajiwa kuachiliwa ambapo pia inasemekana ngoma yenyewe ilifanyika katika studio za FP zilizoko katika mtaa wa mabanda wa Kawangware jijini Nairobi.

Februari 14 usiku, Raila aliweka kwenye mtandao wake wa Twitter na kusema kwamba wimbo wake mpya na msanii Musindi umepikwa na upo tayari kupakuliwa kwa wakenya kesho yake.