Zuchu:Diamond anamjua mpenzi wangu

Muhtasari
  • Katika hafla ambayo ilifahamika kama Mhaba ndi ndi ndi, Zuchu alisema kwamba Diamond anamjua mpenzi wake
ZUCHU
ZUCHU
Image: instagram/zuchu

Msanii Zuchu na staa wa bongo Diamond Patnumz wamekuwa wakivuma kwa muda baada ya uvumi kuenea kuwa ni wapenzi.

Wawili hao walikana madai hayo, huku tarehe 14 Februari ikitarajiwwa na kusubiriwa sana na mashabiki kwani walitarajia mengi kutoka kwa wasanii hao wawili.

Katika hafla ambayo ilifahamika kama Mhaba ndi ndi ndi, Zuchu alisema kwamba Diamond anamjua mpenzi wake.

"Diamond anamfahamu mpenzi wangu."

Alipoulizwa kwanini aliamua kutembea naye kwenye red carpet, Diamond alisema;

“Zuchu ni msanii wangu, si mara ya kwanza kuingia naye kwenye red carpet, mara ya kwanza nilipokuwa namzindua, nilipomleta hapa ni mtoto, sasa hivi ni mkubwa, Mtoto kwa baba hakui."

Diamond ndipo alipoulizwa kama alijua mpenzi huyo ana mpango wa kuchumbiana na Zuchu mwaka huu.

“Wanaopendana wanaweza kufanya mambo mengi, nikiwa kiongozi ni kukubaliana tu na kinachotokea, mradi msanii wangu anafurahi mimi nafurahi,” alisema.

Zuchu aliendelea kumtakia mpenzi wake siku njema ya wapendanao.