Msanii Juma Jux awasili Kenya kwa ziara ya kimuziki

Muhtasari
  • Msanii Juma Jux awasili Kenya kwa ziara ya kimuziki
Juma Jux
Juma Jux

Mwimbaji wa Tanzania Juma Jux amewasili nchini Kenya kwa ziara ya vyombo vya habari nchi nzima ili kuitangaza chapa yake ya 'African Boy'.

Mwimbaji huyo wa Tanzania aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta siku ya Alhamisi asubuhi, kulingana na video iliyoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Pia kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alitangaza kuwa amewasili nchini Nairobi.

Akiongea na waandishi wa habari, Jux alisema kuwa dhumuni lake kuu la kutembelea Kenya ni biasharalakini atatumbuiza mashabiki wake akiwa nchini.

"Kuna kazi nimekuja kufanya na pia nimekuja kwa media tour na pia kuna club appearances," alisema Juma Jux.

Mwimbaji huyo, ambaye anachukulia Kenya kama makazi yake ya pili, alikuwa ametangaza ziara yake nchini Kenya kwenye Instagram yake mapema wiki.

“Niaje niaje watu wangu wa nguvu wa +254, nitatikisa nawe wikendi hii. Imekuwa muda lakini sasa nimerudi kwenye nyumba yangu ya pili siwezi kusubiri kuwaona nyie! I love you is out now...Link ipo kwenye bio. Tupatane hapo hapo au sio #Africanboy #kingofherts,” aliandika Jux.