Najijua, mimi ni player- Diamond Platnumz akiri

Muhtasari

•Staa wa Bongo Diamond Platnumz anasikika akijipiga kifua kuwa ana uwezo mkubwa wa kuvutia wanadada wengi na kuwachezea.

•Mpenzi wake wa zamani Zari Hassan na ambaye ni mama ya watoto wake wawili pia anasikika akimwarifu kuwa alitia doa kwenye mahusiano yao.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Kampuni ya filamu ya Netflix inakaribia kuzindua Reality Show kwa jina 'Young, Famous and African' mnamo tarehe 18 Machi.

Shoo hiyo ambayo imesubiriwa kwa hamu na ghamu itaangazia maisha ya baadhi ya watu maarufu na tajiri barani Afrika wakiwemo Diamond Platnumz kutoka Tanzania, mfanyibiashara Zari Hassan kutoka Uganda, rapa Nadia Nakai na mtangazaji Andile Ncube kutoka Afrika Kusini, waimbaji Annie Macaulay-Idibia na 2Baba kutoka Nigeria kati ya wengine.

Katika kipande kidogo cha shoo hiyo ambacho kilipakiwa mtandaoni Instagram na Zari, wasanii watu waliohusika katika kipindi hicho wanafichua mengi kuhusu maisha yao.

Staa wa Bongo Diamond Platnumz anasikika akijipiga kifua kuwa ana uwezo mkubwa wa kuvutia wanadada wengi na kuwachezea.

"Ninajijua, mimi ni player!" Diamond anasikika akikiri huku akionekana kujivunia jambo hilo.

Mpenzi wake wa zamani Zari Hassan na ambaye ni mama ya watoto wake wawili pia anasikika akimwarifu kuwa alitia doa kwenye mahusiano yao.

"Uliharibu!" Zari anasikika akimwambia Diamond katika video hiyo.

Katika shoo hiyo Diamond pia anakiri kwamba kuwa mtu maarufu, tajiri na mwenye umri mdogo ni jambo nzuri sana.

Diamond ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ubabe wake katika muziki wa Bongo anaaminika kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya wanawake kumi kutoka mataifa mbalimbali.

Miongoni wao ni Hamisa Mobetto, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Zari Hassan, Tanasha Donna na wengineo.  Hivi majuzi alikiri kuwa kwenye mahusiano mengine kwa sasa ila hakufichua jina la mchumba wake.