Nipo tayari sasa kwa tuzo za BET - Christina Shusho

Muhtasari

• Msanii wa miziki ya injili kutoka Tanzania, Christina Shusho amesema kwamba yupo tayari na anajiandaa kwa tuzo za BET.

• Aidha msanii huyo amesema kwamba kwa sasa analenga zaidi kuwashirikisha wasanii kutoka taifa la Congo katika kazi zake, ili kusukuma muziki wake nje ya Tanzania.

Christina Shusho
Christina Shusho
Image: Instagram, KWA HISANI

Msanii wa miziki ya injili kutoka Tanzania, Christina Shusho amesema kwamba yupo tayari na anajiandaa kwa tuzo za BET.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Presenter Ali, Shusho amesema kwamba kwa sasa tayari ameshashinda tuzo nyingi za ndani ya Tanzania na hata ukanda wa Afrika mashariki ila kwa sasa anaazimia kuwania tuzo za kimataifa kama BET.

Aidha msanii huyo amesema kwamba kwa sasa analenga zaidi kuwashirikisha wasanii kutoka taifa la Congo katika kazi zake, ili kusukuma muziki wake nje ya Tanzania.

Shusho amesema kwamba kwa sasa anaandaa album yake na maandalizi yake yanaelekea kukamilika, huku akisema kwamba mashabiki wake watarajie kazi nzuri na tofauti kutoka kwa album hiyo.

Ametoa shukrani zake kwa wakenya ambao wamempa sapoti tangu anaanza muziki na kusema kwamba atazidi kuwabariki na kazi nzuri.

Mwanamuziki huyo ni mmoja kati ya wasanii wa miziki ya injili ambao wanaheshimika na kupendwa na wengi, la mno kwa sasa likiwa kusubiria ngoma zitakazododndoka kutoka kwa album yake.