Redsan ashinda tuzo ya Lifetime Achievement Award

Muhtasari

• Redsan ang'ara katika usiku wa kutoa tuzo ambapo amesherehekewa kama mwanamuziki aliyedumu zaidi kwenye sanaa, Lifetime Achievement Award.

Redsan
Image: Instagram

Mwanamuziki mkongwe wa dancehall nchini Kenya, Redsan ni mtu mwenye furaha baada ya juhudi na jitihada zake za muda mrefu kwenye Sanaa ya muziki nchini Kenya kutambulika na kutuzwa.

Msanii huyo amejishindia tuzo ya Lifetime Achievement Award katika tamasha ya kupeana zawadi iliyoandaliwa katika mgahawa wa Nairobi Street Kitchen usiku wa Alhamisi 24.

Tuzo hizo zilizokuwa zitolewa na Pulse Music Video Awards, kwa mara ya saba tangu ziasisiwe ziliona wasanii mbalimbali wakituzwa katika vitengo mbalimbali kwa Sanaa ya muziki nchini.

Redsan ambaye amedumu kwa Sanaa kwa Zaidi ya miaka 25 aliipokezwa tuzo hiyo kwa mihemko mikali, tuzo ambayo ilikuwa inasherehekea kazi zake za muziki na jinsi ambavyo amekuwa akichangia katika Sanaa hiyo nchini Kenya kwa muda huo wote.

Msanii huyo akiandika kwenye Instagram yake amewashukuru wote pamoja na waandalizi wa tuzo hizo kwa kumuaminia nqa kumchagua kwa tuzo hiyo.

"Ahsante sana Pulse Award kwa kutambua jitihada zangu na kwa uhakika ninashukuru sana kwa utambuzi wenu. Hii ni hatua muhimu katika taaluma yangu na nimenyenyekea na kuheshimiwa kupokea tuzo hii. Asante kwa mashabiki wangu wote ambao wamekuwa wakiunga mkono harakati kutoka siku ya kwanza," aliandika Redsan

Wasanii wengine ambao waling’ara katika tuzo hizo ni Nikita Kering, Iyanii, Wanavokali miongoni mwa wasanii wengine wengi nchini Kenya.

Redsan anapokezwa zawadi hii ya kuchangia pakubwa katika Sanaa ya muziki nchini Kenya, siku chache tu baada ya wasanii chipukizi kumsuta kwamba katika muda wake mrefu kwenye Sanaa, Redsan hajasaidia msanii hata mmoja anayechipukia ambapo nguli huyo wa dancehall aliwajibu kwa kuwaambia kwamba hawezsi saidia kila mtu kwa sabqabu yeye si shirika la dunia la utoaji misaada, UNICEF.