Jimal afunguka kuhusu hali ya afya ambayo amekuwa akipambana nayo tangu shule ya upili

Muhtasari
  •  Marlow alishiriki chapisho refu kwenye mitandao yake ya kijamii akifichua hali ambayo amekuwa akipambana nayo

Mwenyekiti wa Nairobi Matatu Sacco, Jimal Roho Safi amefunguka kuhusu hali ya kiafya ambayo amekuwa akipambana nayo tangu alipokuwa katika shule ya upili.

Tajiri huyo wa Nairobi alishiriki chapisho akizungumzia hali yake.

JImal amekuwa akijulikana kwa muda sasa. Hii ni tangu aanze kuchumbiana na mwanasosholaiti Amber Ray.

 

 Marlow alishiriki chapisho refu kwenye mitandao yake ya kijamii akifichua hali ambayo amekuwa akipambana nayo.

Marlow alidai kuwa amekuwa akipambana na kukosa usingizi tangu alipokuwa katika shule ya upili.

Kwenye chapisho hilo, mfanyabiashara huyo alisema kuwa hajawahi kulala kwa zaidi ya saa tano tangu maisha yake ya shule ya upili.

Mfanyabiashara huyo aliendelea na kufichua kwamba alilala saa 11 jioni na kufikia 2:30 asubuhi alikuwa tayari ameamka. Wanamtandao wamemhimiza atafute matibabu.